Saturday, November 9, 2013

(i) NYANYA.
Baada ya kutoa maelezo ya jumla kuhusu kilimo cha mboga katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii, nilisema kwamba mboga huwekwa katika makundi matano, yaani Matunda, Majani, Mizizi, Mashina na Maua. Mboga hizi nitazieleza kwa kufuata makundi zilimowekwa.
Leo tutaanza na Nyanya katika kundi la Matunda.

Nyanya ni mboga inayolimwa na kuliwa kwa wingi hapa nchini kwetu Tanzania na duniani kote kuliko aina nyingine yoyote ya mboga. Nyanya huweza kuliwa zikiwa mbichi, au kupikwa na kuwa mchuzi au supu. Vile vile ni kiungo kikubwa ktk mapishi mbali mbali ya vitoweo na michuzi. Pia Nyanya hutumika ktk kutengeneza masala, siki, kachumbari na kadhalika. Mikoa inayolima kwa wingi Nyanya ni Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa na Mbeya, na kiasi flani kanda ya ziwa hasa Mwanza, Musoma na Bukoba.

(a) AINA ZA NYANYA.
Ziko aina nyingi za Nyanya. Hata hivyo, kiasi cha aina 10 hadi 15 ndizo zilimwazo kwa wingi zaidi.
Katika kuchagua aina za kupanda ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
(i) Sababu ya kustawisha nyanya; kula au kuuza.
(ii) Muda uliopo wa kuzistawisha.
(iii) Wingi wa mavuno.
(iv) Ustahimilivu wa magonjwa na kutopasukapasuka.
(v) Umbo la sura yake.
Miongoni mwa aina za Nyanya ambazo hustawishwa sana na wakulima wetu ni Money Maker, Marglobe, Rutgers, Amateur, Potentate, Oxheart, Earliana, Urbana na Best of All.
(b) HALI YA HEWA.
Nyanya hupendelea hali ya joto, lakini kukiwa na unyevu wa kutosha ardhini. Mvua nyingi husababisha mimea kushambuliwa na magonjwa. Upepo mkali husababisha kupukutika kwa maua na hatimaye kupungua kwa mavuno.
(c) HALI YA UDONGO.
Nyanya huweza kustawi ktk aina nyingi za udongo. Hata hivyo udongo mwepesi au ulio nusu kichanga na nusu mfinyanzi ndio ufaao zaidi. Zao hili halipendelei ardhi yenye maji maji, lakini ni muhimu kuwepo na unyevu wa kutosha ktk muda wote wa kukua.
Makala hii itaendelea katika kipindi kinachofuata ktk sehemu hii ya pili na nitaeleza kwa undani magonjwa ya nyanya, wadudu na tiba yake.
Stay tuned Mkulima uelimike.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete