Sunday, November 10, 2013

(ii) BILINGANYA

Zao hili hustawi zaidi katika nchi za joto, hasa kusini mwa Asia, Mashariki ya Mbali na Afrika.

(a) AINA ZAKE
Kama ilivyo kwa mazao mengine, ziko aina nyingi za bilinganya ambazo hutambuliwa kwa tofauti za maumbile, sura na rangi na hujulikana kwa majina mbali mbali. Aina zinazojulikana zaidi ni: Black Beauty na Early Purple, ambazo ni za mviringo na: Florida High na Sadohara Purple, ambazo ni ndefu nyembamba.

(b) HALI YA HEWA
Bilinganya ni mmea uchukuao muda mrefu kukua, na hauna nguvu nyingi. Huhitaji hali ya joto katika muda wote wa kustawi. Baridi kali huweza kudumaza na pengine kuua mmea.

(c) HALI YA UDONGO
Zao hili huhitaji udongo laini na unyevu wa wastani. Ardhi iwe na rutuba ya kutosha, na kila inapowezekana ni bora kutumia samadi au mbolea ya takataka. Utayarishaji wa ardhi na bustani ni kama vile kwa mazao mengine ya mboga.

(d) KUPANDA NA KUTUNZA.
Kwa kawaida mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma 8 hadi 10. Kisha miche hung'olewa na kupandikizwa kwenye bustani.
Umbali wa kupanda miche ni sentimeta 60 hadi 90 kati ya mmea, na sentimeta 90 hadi 120 kati ya mistari. Unatakiwa kutifuatifua udongo wa juu mara kwa mara na kila inapolazimika uongezaji wa maji licha ya kutegemea mvua.

(e) MAGONJWA
Kuna magonjwa makubwa mawili ya zao hili, nayo ni:
Fruit Rot: Ugonjwa huu husababishwa na vimelea na hushambulia sehemu zote za mmea isipokuwa mizizi. Majani huwa na madoa ya hudhurungi. Mashina (hasa ya miche michanga) hushambuliwa, na mara nyingi huoza. Matunda nayo hupata madoa hatimaye sehemu zenye athari hiyo hulainika na kuoza. Hakuna dawa maalum ya kuzuia, inashauriwa kubadilisha mpando na kupanda aina zenye uvumilivu.
Wilt: Dalili za ugonjwa huu ni kwamba rangi ya majani hugeuka njano, halafu hupukutika kidogo kidogo. Mimea hudumaa na kufa kabla ya kukomaa

(f)WADUDU
1. Beetles na Aphids- huathiri mimea michanga
2. Lacebug- hufyonza utomvu wa mmea
Kwa wadudu hawa wote, tumia sumu yoyote kama Malathion 5%, Thiodane n.k

Bilinganya husaidia kulainisha usingizi.

0 comments:

Post a Comment