Tuesday, October 18, 2016

Mahindi ni zao linalolimwa katika maeneo mengi hapa nchini, linahimili katika udongo wenye uchachu wa 6-6.5. Hustawi zaidi kwenye maeneo yenye mwinuko wa 2500. Zao la mahindi kama mazao mengine lina kanuni Zake.

KANUNI YA KWANZA: KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA.

Tayarisha shamba la mahindi mara tu baada ya kuvuna mazao ya msimu uliopita. Mahindi hustawi sehemu yenye udongo wenye rutuba na usiosimamisha maji. Moto usitumike Kuandaa shamba.

FAIDA ZA KUTAYARISHA SHAMBA MAPEMA.

Baada ya kuvuna,udongo bado ni mlaini hivyo hulimika kwa urahisi kwa kutumia jembe lolote. Masalia yatakayofunikwa udongoni huoza mapema. Hupunguza magugu. Hupunguza wadudu waharibifu.

KANUNI YA PILI: KUPANDA.

Wakati wa kupanda hutatanisha kwani mvua hayatabiriki,Kama mvua hunyesha nyakati na majira yale yale ya mwaka basi kalenda ifuatayo inaonyesha tahere za kupanda zao la mahindi katika eneo lako. Mbeya na maeneo ya jirani, mwanzoni mwa mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni. Morogoro na maeneo ya jirani, Mwezi Januari katikati hadi Februari katikati Iringa na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Desemba mwishoni Songea na maeneo ya jirani, katikati ya mwezi Novemba hadi Januari mwanzoni. Kupanda mahindi mapema ni muhimu kwani uwezekano wa kuvuna mazao mengi ni mkubwa. Kwa mashamba makubwa makubwa sana wakati wa kupanda uwe wiki moja kabla ya mvua kuanza kunyesha na isizidi wiki mbili kabla ya mvua. Isiwe mapema zaidi kwani mbegu zitaharibiwa na joto kati ya udongoni wadudu,panya,ndege na wanyama wengineo.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA.

Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa. Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo. Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

KANUNI YA TATU: KUCHAGUA MBEGU BORA.

Mbegu bora ni zile zilizo zalishwa kitaalamu. Ni safi hazijabunguliwa na wadudu. Huzaa mazao mengi. Hustahimili magonjwa.

AINA ZA MBEGU.

1. Mbegu aina ya chotara (hybrid).
2. Aina ya ndugu moja(synthetic).
3. Mbegu aina ya composite.

Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika misingi ya kilimo, zina uwezo wa kuzaa magunia 50-80 au tani 5.5 – 7.5 kwa hekta moja au gunia 20-35 kwa hekari.

MAPENDEKEZO YA MBEGUZA KUPANDA.

Kuna mbegu nyingi za kisasa zilizoko kwenye soko mfano SIDCO ,PANNAR, PIONEER, KITALE kutoka KENYA n.k.
Ni vyema kufuata ushauriwa wataalamu wa kilimo.

KANUNI YA NNE KUPANDA.

Idadi ya mimea katika eneo ni muhimu kwani uzoefu unaonyesha wakulima wengi hawapati kiwango kinachotakiwa kutokana na upungufu wa idadi ya miche katika eneo husika. Na athari zake ni:-
1. Mazao hupungua.
2. Mmea huangushwa na upepo Mabua mengi hayazai. 3. Idadi ya mimea nayo ikipungua kwenya eneo husababisha mavuno kupungua jambo la kufanya ni kupanda mbegu katika nafasi sahihi zilizoshauriwa na wataalamu na kupanda kwa wakati na kwa umakini.

KIASI CHA KUPANDA.

Mbegu za mahindi huhifadhiwa kwa dawa kali na kiasi cha 10kg hutosha kupanda ekari moja. Nafasi za kupanda. 75cm x 30cm mche mmoja 75cm x 60cm miche miwili 90cm x 45cm miche miwili

KANUNI YA TANO; KUTUMIA MBOLEA.

Mahindi hustawi na kuzaa vizuri iwapo yatapatiwa mbolea pamoja na matunzo mengine ya kilimo bora. Ukipanda mbegu bora bila kutumia mbolea ni kazi bure.

KUNA AINA KUU MBILI ZA MBOLEA.

1. Mbolea za asili mfano; samadi,mboji na majani mabichi,mbolea hizi hazina virutubisho vya kutosha.
2. Mbolea za viwandani; ambazo hizi zimegawanyika katika makundi mawili ambayo ni za Kupandia na za kukuzia.

KANUNI YA SITA: KUVUNA KWA WAKATI.

Ili kuhakikisha upatikanaji wa kipato cha kutosha, ni lazima kuhakikisha kuwa mahindi yanavunwa kwa wakati. Utafiti unaonyesha kuwa 30% ya mavuno hupotea katika mchakato wa uvunaji, usafirishaji mpaka sokoni. Kwa ni muhimu sana kufuata njia bora na sahihi za uvunaji.

Ahsanteni............

Prepared by:

Marcodenis E. Misungwi. Agriculture Extensionist.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete