Wednesday, October 19, 2016

Ng'ombe hutoa maziwa lakini pia hutoa mazao mengine kama ngozi,mbolea na hutumika kama wanyama kazi. Zaidi ya asilimia 95 ya ng,ombe hutumika kama wanyama kazi.

Zaidi ya asilimia 95 ya ng’ombe wanaofugwa hapa nchini ni wa asili ambao huzalisha nyama na maziwa kwa kiwango kidogo ikilinganishwa na wale wachache walioboreshwa. Ng’ombe walioboreshwa wamegawanyika katika makundi mawili.
.Wale wanaofugwa kwa ajili ya nyama na wanaofugwa kwa ajili ya maziwa.

Ili kuwawezesha ng’ombe kuzalisha mazao bora ya nyama, maziwa na ngozi mfugaji anapaswa kufuata kanuni za ufugaji bora ambazo ni pamoja na:-

Kufuga ng’ombe katika eneo kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho katika mfumo wa ufugaji huria.
1. Kujenga banda au zizi bora.

2. Kuchagua koo/aina ya ng’ombe kulingana na uzalishaji (nyama au maziwa).

3.Kutunza makundi mbalimbali ya ng’ombe kulinga na umri na hatua ya uzalishaji.

4. Kumpa ng’ombe lishe sahihi kulingana na umri na mahitaji ya mwili.

5. Kudhibiti magonjwa ya ng’ombe kama inavyoshauriwa na mtaalamu wa mifguo.

6. Kuvuna mifugo katika umri na uzito muafaka kulingana na mahitaji ya soko.

7. Kuzalisha maziwa, nyama na ngozi zinazokidhi viwango vya ubora na usalama.

8. Kutunza kumbukumbu za uzalishaji na matukio muhimu ya ufugaji.

MIFUMO YA UFUGAJI.

Ng’ombe wanaweza kufugwa katika mfumo wa ufugaji huria au kulishwa katika banda (ufugaji shadidi).

Ufugaji huria huhitaji eneo kubwa la ardhi yenye malisho mazuri na vyanzo vya maji. Pamoja na kuwa na ufugaji huu, ni muhimu ardhi hiyo itunzwe kwa kuzingatia uwiano wa idadi ya ng’ombe na malisho. Ufugaji wa shadidi uzingatie uwepo wa banda bora na lishe sahihi.

UFUGAJI KATIKA MFUMO HURIA.

Ili mfugaji aweze kupata mazao mengi na bora katika ufugaji huria anapaswa kuzingatia yafuatayo:-

1. Atenge eneo la kutosha la kufugia kulingana na idadi ya ng’ombe alionao.

2. Atunze malisho ili yawe endelevu na yapatikana wakati wote.

3. Awe na eneo lenye maji ya kutosha na Atenganishe madume na majike ili kuzuia ng’ombe kuzaa bila mpangilio.

Matunzo mengine ya ng’ombe yazingatie vigezo vingine muhimu kama;
   - umri,
    - hatua ya uzalishaji
     - matumizi ya ng’ombe      husika.

BANDA/ZIZI BORA LA NG’OMBE BANDA BORA.

Banda lijengwe sehemu ya mwinuko mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo; 

1. Uwezo wa kumkinga ng’ombe dhidi ya mvua, upepo, jua kali na baridi.

2. Kuta imara zenye matunda au madirisha kwa ajili ya kuingiza hewa na mwanga wa kutosha, Sakafu yenye mwinuko upande mmoja ili isiruhusu maji na uchafu kutuama.

3. Lijengwe katika hali ya kuruhusu kufanyiwa usafi kwa urahisi kila siku, na sakafu ngumu ya zege au udongo ulioshindiliwa na kuweka malalo.

4. Paa lisilovuja.

Aidha kwa wafugaji wanaofuga katika ufugaji huria ambako mazizi hutumika, inashauriwa kuzingatia yafuatayo:-

1.Zizi likae mahali pa mwinuko pasiporuhusu maji kutuama.

2. Zizi liweze kukinga mifugo dhidi ya wezi na wanyama hatari.

2. Ukubwa wa zizi uzingatie idadi na umri wa mifugo ng’ombe watengwe kulingana na umri wao.

3. Zizi lifanyiwe usafi mara kwa mara na Liwe na sehemu ya kukamulia (kwa ng’ombe wa maziwa), stoo ya vyakula, sehemu ya kutolea huduma za kinga na tiba, eneo la kulishia na maji ya kunywa.

ZIZI BORA.

Zizi lijengwe sehemu ya mwinuko isiyoruhusu maji kutuama mbali kidogo na makazi ya watu na liwe na sifa zifuatazo:-

1.Liweze kuhakikisha usalama wa ng’ombe. Ukubwa wa zizi uzingatie idadi ya mifugo.

2. Liwe na sakafu ya udongo ulioshindiliwa vizuri na kufanyiwa usafi mara kwa mara.

3. Zizi la ndama liwe na paa ma Lijengwe kwa vifaa madhubuti na visivyoharibu ngozi.

KUMBUKUMBU NA TAKWIMU MUHIMU.

Kumbukumbu ni taarifa au maelezo sahihi yaliyoandikwa kuhusu matukio muhimu ya kila ng’ombe na shughuli zote zinazohusiana na ufugaji. Mfugaji anashauriwa kuweka kumbukumbu na takwimu muhimu katika shughuli zake za ufugaji wa ng’ombe. Kumbukumbu zinamsaidia mfugaji kujua mapato na matumizi na kufanya maamuzi sahihi kuhusu mifugo husika na mazao yake. Aidha humwezesha kuweka mipango ya shughuli zake. Mfugaji anapaswa kuweka kumbukumbu muhimu zifuatazo:-

1. Uzazi (uhamilishaji na matumizi ya dume, tarehe ya kupandwa, kuzaa na kuachisha kunyonya)

2. Kinga na tiba

3. Utoaji wa maziwa

4. Ukuaji

5. Idadi ya ng’ombe kwa makundi – majike, ndama, mitamba, madume,maksai.

Ahsanteni

Prepared by:

Marcodenis E. Misungwi

Agriculture Field Extensionist.

0 comments:

Post a Comment