Wednesday, December 25, 2013

HISTORIA YA KRISMASI

Ndugu zangu leo ni Krismas, ni sherehe zinazoazimishwa kila mwaka tarehe kama ya leo mwezi kama huu 25  Desemba. Sherehe hizi ni za kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristu kama inavyojulikana. Sherehe hizi zinaazimishwa na Wakristu karibu wote duniani isipokuwa Waadventista Wasabato ambao wanaamini katika Biblia. Hebu tujiulize je sherehe hizi ni za kidini au zimeanzishwa na binadamu?

  Wakati wa zama za kale , siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za kusini kulisheherekewa mfano wa usiku ambao mungu wa mama watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni Mungu wa jua.Pia siku hii inaitwa Yule, siku ambayo inasheherekewa  mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira baridi.

Wakati wa Warumi, iliazimishwa kwa kumsifu Satanusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mwaliko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.

  Siku ya mwisho ya majira ya baridi  huko sehemu za mviringo za kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Disemba.

Wakristu wa kale

Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristu wa kale walikaa majumbani  mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya wakristu iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shurti za kikristu. Lakini makanisa ya kale hakika hayakusheherekea mwezi Disemba kwa kuzaliwa Kristu hadi alipokuja Telesforusi ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136, askofu huyo ndiye aliyetangaza  kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha "kuzaliwa kwa Bwana wetu wa Mwokozi". Hata hivyo kwa vile hakuna mtu  hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo,  kawaida ya Uzawa  ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa sherehe za Kiyahudi za Trumpetse (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300,  watu waliewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.

  Katika mwaka 274, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Disemba. Mfalme wa Roma aitwye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni "Natalis Solis Invict", 'Sherehe ya kuzaliwa Jua lisiloshindikana'.
Katika mwaka 320, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Disemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristu.

  Mnamo mwaka 325, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa  maanani. Mtakatifu Constatine, ambaye ni mfalme wa mwanzo wa dhehebu la ukristu la kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika  kwa tarehe 25 Disemba. Pia aliitanguliza  Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza  Pasaka kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusheherekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Disemba.

  Hata hivyo, ingawa, Costantine aliifanya rasmi tarehe 25 Disemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitmbua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni.
Hata hivyo bado krismasi haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800.

Krismasi inaanza kuwa maarufu

Umaarufu wa krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820, ulianza ghafla mnamo mwaka 1820. Ilikuja kuwa maarufu ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la kwanza ndani ya marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwaYesu.

Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya kikristu yananasibiwa ndani ya Krisimasi. Kulingana na nyakati katika Biblia, Yesu alizaliwa mwezi Machi, bado yake ya kuzaliwa inasheherekewa Disemba 25. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za krismasi (Disemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisheherekewa na wapagani wa ki-rumi wa kale kwa kuadhimisha kurudi kwa Jua.

Je, Krismasi ina ushahidi wa ki-biblia?

Neno 'Krismasi' halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kwa kimoja; upambaji wa mti. Biblia yenyewe inashutumu upambaji wa mti (ya krismasi):  "Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaunganisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika" (Jeremia 10-3,4).

Ndugu zangu, tunapoendelea kusheherekea Krismasi, tujiulize swali hilo la 'Je, Krisimasi ni sherehe za kidini?'   Ahsanteni sana na Sikukuu Njema.

0 comments:

Post a Comment