Sunday, December 29, 2013

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kimehadhalisha walaji wa nyama ya Nguruwe nchini kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa. Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA umebaini kuwa baadhi ya Nguruwe wana minyoo aina ya Tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Mhadhiri na Mtafiti Idara ya sayansi ya Wanyama na Uzalisha ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya zimebaini Nguruwe wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Prof. Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia mradi wa utafiti wa kuboresha ufugaji wa Nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya Nguruwe kwa ajili ya vipimo. "Majibu ya Sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa Nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na serikali" alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya Nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha Nguruwe kujitafutia chakula na maji mitaana na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Prof. Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha Nguruwe kutafuta malisho ktk vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao. Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambukizi hayo inaweza kutokea ktk miji mikubwa ikiwamo Dar es salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo. "Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu" alisema Profesa Lekule.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete