Thursday, December 19, 2013

Habari ya siku mbili tatu ndugu zangu wakulima, ni kama siku tano sasa sijawawekea chochote humu. Ni majukumu tu yalinizidi wakulima wenzagu.
Leo hii nataka niwashirikishe jambo moja, na jambo hili inabidi kila mmoja wetu ajiulize swali hili "Je, Mahafali ya Mkulima Mdogo Mdogo ni Lini?" Kila mkulima ajiulize yeye ni mkulima wa aina gani, je ni mdogo, ni wa kati au ni mkubwa? Kama ni wa kati, je umesheherekea mahafali ya kuhitimu na kuwa mkulima mkubwa?

Leo hebu tumjadili huyu mkulima mdogo, ambaye ndiye anayechukua asilimia kubwa ya wakulima wa nchi yetu Tanzania, ambaye ndiye aliye kwenye sekta inayoajiri watu wengi kuliko sekta zote nchini, zaidi ya 75%.

Mkulima huyu tangu enzi anaitwa mkulima mdogo mdogo, viongozi wa serikali na wanasiasa wanaimba kila siku "kumsaidia mkulima mdogo mdogo". Sasa basi tuangalie huyu mkulima mdogo mdogo (small holder farmer) anafanya yeye kama yeye na anawezeshwa kwa dhati kwamba atoke alipo? Au amewekwa kama daraja la kuvukia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa manufaa ya vitu vingine tofauti na yeye?

Leo hebu tuangalie sehemu moja, Serikali, katika kumsaidia huyu Mkulima Mdogo (small holder farmer) ili aweze kutoka hapo alipo na apande daraja lingine la juu zaidi.
Ni kweli serikali ina jukumu la kuajiri mabwana shamba ambao ndio wanafanya kazi karibu kabisa na Mkulima huyu, lakini huyu Bwana Shamba anaifanya kazi kwa dhati na moyo mmoja? Je, amepewa vitendea kazi? Jibu sahihi ni kweli kuna ambao ni mzigo kwa Mkulima, lakini wapo wanaoifanya kazi yao kwa moyo mmoja na bidii zote kakini wanakwamishwa na ukosefu wa vitendea kazi.

Serikali ndie mhimili wa kila kitu ktk nchi. Kuna Msaada serikali iliupokea kutoka Japani wa mbole ya kupandia aina ya DAP tani 6003.8, ikimulenga mkulima mdogo mdogo, cha kushangaza anayelengwa hajaambiwa, haijatangazwa utaratibu wake, imeonekana sokoni tu ikiuzwa, ambapo inawezekana mlengwa isimfikie maana hajui chochote. Picha hapo juu inamuonyesha waziri wa kilimo akizipokea!

Tujiulize, huyu mkulima atahitimu lini?

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete