Monday, December 2, 2013

(i) RADISHI.

Zao la radishi hujulikana pia kama "Karoti Nyeupe", hupendwa sana na wakulima kwa sababu hustawishwa kwa urahisi na hukua haraka na kutumiwa katika muda mfupi. Asili ya zao hili ni katika nchi za Ulaya.

Ijapokuwa radishi hasa ni zao la nchi za baridi, siku hizi linastawishwa zaidi katika nchi zenye joto la kadri (Temperate zone) na katika Nyanda za juu za tropiki.

AINA: Kuna aina nyingi za radishi ambazo hutofautiana kwa umbo, ukubwa na rangi ya matunda (mizizi) yake. Aina zinazojulikana zaidi ni Chery Belle, Comet, Scarlet Globe, Sparkler, White Icicle, White Chinese, Golden Globe, French Breakfast na Sakurajima.

Mmea wa radishi ni wa msimu mmoja, lakini katika nchi za baridi mmea huu huweza kukua kwa kipindi kirefu zaidi na kutoa shina au mlingoti wenye vitawi. Chakula aina ya wanga kitengenezwacho na mmea hulundikana kwenye mzizi na kuuvimbisha. Umbo la mzizi huwa mviringo, au mviringo uliochongoka kidogo, au refu mfano wa pingili. Rangi yake ya nje ni nyekundu, au zambarau, au nyeusi, au rangi ya maziwa (cream), lakini kwa kawaida rangi ya ndani ni nyeupe. Mzizi huliwa ukiwa mbichi au baada ya kupikwa, pia majani yake huweza kupikwa na kutumiwa.

USTAWISHAJI: Zao hili huweza kuoteshwa katika aina nyingi za udongo, lakini hustawi vizuri mahali penye ardhi laini, tifutifu, au nusu kichanga mradi pawepo na rutuba ya kutosha.

Radishi hupendelea hali ya ubaridi wa kadiri, hivyo katika nchi za tropiki unashauriwa kulima zao hili katika sehemu za milimani ambako joto lake siyo kali.

KUPANDA: Radishi ni mmea wenye uwezo wa kustawi bila shida, na unaweza kuoteshwa karibu wakati wote wa mwaka. Ni vizuri mipando ya zao hili iachane kwa kipindi cha majuma mawili hivi kusudi uweze kupata mboga zake wakati wote.

Mbegu zake hutiwa kidogo kidogo katika mistari yenye kina cha sentimeta 1 hadi 2, kisha hufunikwa kidogo kwa udongo laini. Kilo 3 za mbegu hutosha robo hekta ya bustani, umbali wa mistari ni sentimeta 30 hadi 40. Baadaye miche hupunguzwa na kuacha nafasi ya 5-8 sentimeta.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete