Friday, November 8, 2013

Ndugu zangu wakulima, nafahamu kwamba mnajiandaa na msimu wa kilimo sasa. Na najua pia changamoto mnazokumbana nazo kwenye maandalizi ya kuhudumia mashamba yetu, na kati ya mahitaji makubwa ni mbolea.
Wakati kama huu ndio wa kuwa makini sana hasa katika suala la uandaaji wa mbolea maana wapo watu ambao hutumia fursa hii kupita kwa wakulima na kuwahadaa, lengo lao likiwa ni kujipatia kipato.
Kuna watu wanapita pita sana wakitangaza na kunadi mbolea moja hivi ya maji, "Super Gro" watu hawa wanatoka katika shirika la GNLD, wanapita sana huku wilayani mbozi hasa katika kata za Isansa, Igamba na Msiya.
Mimi binafsi nimekutana watu hao, nilipewa taarifa na mtendaji wangu kwamba kuna wageni wanakuja na kazi yao hasa ni kukutana na kuongea na wakulima, wanatangaza na kuuza mbolea yao ijulikanayo kama super gro. Mimi kama mtaalamu wa kilimo niliwaeleza na kuwaandaa watu kwa kusaidiana na mtendaji wangu. Siku ikafika ya ujio huo. Alikuja dada mmoja na kuanza kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi na faida za mbolea hii ya maji, wakamsikiliza. Alipomaliza wakulima wakamuuliza maswali, katika maswali ndipo nilipopata mashaka na ujio huo ikabidi nifuatilie kwa undani mchakato na uhalisia wa mbolea hii.
Kwanza ki uhalisia hii siyo mbolea kwa ajili ya nafaka maana haina kirutubishi hata kimoja kinachofaa kwa Mhindi na mazao mengine ya nafaka, ni kirutubishi cha majani tu na si punje, inafaa kwenye mboga mboga.
Viambata(ingredients) yake ni kama ifuatavyo;

1. Ethoxylated- chemical hii inatumika inapunguza uwezekano wa maji kupotea, inatunza unyevunyevu (surfactants).

2. Alkylphenols- kiambata hiki kinatumika katika viwanda vya sabuni(detergents) na bidhaa za kusafishia(cleaning products).

3. Polysiloxane- inatumika kwenye viwanda vya plasitic(polymers).

Kwa maelezo yake ni kwamba unapandia mpaka kukuzia, hauhitaji kuweka mbolea nyingine, acha mkulima, hii si mbolea, itumie tu kwa kurutubisha na kustawisha majani na endelea kutumia mbolea za kawaida kama kawaida.
Huo ni ushauri wangu kwako mkulima.
Ahsante!

8 comments:

  1. Mkuu vipi mbolea hii ya supergrow kwa kuku inaweza kufaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapana haiwezekani Mbolea ni kwa mimea pekee

      Delete
    2. INAWEZEKANA 100%

      WEWE ULISHAJARIBU UKAONA KUKU WAKO WANAKONDA AU WANAKUFA..ACHENI KUPOTOSHANA

      ATAESAIDIKA NA M
      KIRUTUBISHO NA ASAIDIKE SIO MPAKA MSAIDIKE WOTE

      Delete
  2. Hapana kwanza hii siyo mbolea kweli Kama alivyosema huyo na wengi wanashindwa kuielezea vizuri kwa tamaa zao za kipesa na ukiona umetumia super grona hujapata matokeo my dear hiyo siyo super gro watu wengi sana wanauziwa vitu vya ajabu na wanaambiwa ni super gro na super gro HAITUMIKI KWA WANYAMA NI KWA AJILI YA MIMEA TU.
    ndugu mpendwa kwa maelezo zaidi 0744041289

    ReplyDelete
  3. Super gro sio mbolea bali ni kurutubisho na ni natural ina tumika kuboresha mazao shambani
    Kwenye bustani na hata kwa mifugo kama samaki na kuku huchanganywa kwenye maji wanayo tumia

    ReplyDelete
    Replies
    1. How comes the plant's food become animal feed or supplement?, Can discuss more

      Delete
  4. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete
  5. He super group huongeza mazao?

    ReplyDelete