Thursday, January 16, 2014

KANUNI YA KWANZA.

Kuotesha mbegu katika kitalu

Tengeneza matuta yenye upana wa mita 1 na urefu wowote kutegemea na mahitaji yako.

Weka mbolea ya samadi ndoo moja hadi mbili kwa mraba wa mita moja.

Lima tuta kiasi cha sentimita 10-25.
Sia mbegu katika mistari yenye nafasi ya sentimita 15 kutoka mstari hadi mstari. Gramu 5 (kijiko cha chai) zinatosha kusia eneo la mraba mita moja.
Tandaza nyasi na mwagilia.

KUMBUKA: Kilo 2.5 za mbegu zinatosha hekta moja ya shamba.

KANUNI YA PILI

Kupanda miche kwa nafasi.

Pandikiza miche katika nafasi ya sentimita 30 kutoka mstari na mstari na sentimita 10-25 toka mche hadi mche.

KUMBUKA: Pandikiza miche wakati wa asubuhi au jioni na mwagilia maji ya kutosha.

KANUNINI YA TATU

Weka mbolea.

Weka mbolea ya kukuzia katika wiki ya nne hadi sita baada ya kupandikiza. Weka mbolea kwenye mstari na hakikisha isigusane na mimea. Hakikisha udongo una unyevu wa kutosha wakati wa kuweka mbolea. Tumia UREA au SA.

KANUNI YA NNE

Kupalilia

Hakikisha shamba linakuwa safi. Wakati wa kupalili, mkulima asichimbue sana udongo ili kuepuka mikwaruzano kwenye shina la vitunguu. Inulia udongo kwenye mashina kama mkulima amepanda sesa.

KANUNI YA TANO

Kuzuia magonjwa/wadudu

Magonjwa ya ukungu ni magonjwa yanayoishambulia mimea ya vitunguu. Magonjwa hayo ni Down Mildew, ugonjwa wa kuvu, kuoza kwa vitunguu.

KUZUIA

Tumia dawa zenye mchanganyiko wa copper mfano Dithane m45, Ivory na Koside. Epuka mikwaruzo/vidonda kwenye vitunguu na pia fuata kanuni za mzunguko wa mazao (crop rotation).

Wadudu waharibifu:

Wadudu wa manjano (Onion thrips). Zuia wadudu hawa kwa kutumia dawa za viwandani kama Actellic 50EC, Selecron na pia madawa ya wadudu yanayopatikana kwenye maduka.

KANUNI YA SITA

Kuvuna kwa wakati

Vuna vitunguu baada ya miezi 4-5 kutegemeana na mbegu iliyopandwa.

Ucheleweshaji wa uvunaji unasababisha vitunguu kuoza na kuharibikia shambani.

KUMBUKA: Tumia jembe la mkono na hakikisha vitunguu havikwaruzwi wakati wa kuvuna. Mkulima anaweza kuvuna tani 30-40 kwa hekta.

HAPPY NEW YEAR!

0 comments:

Post a Comment