Saturday, January 11, 2014

Utupa unaojulikana kwa jina la kitaalamu kama (Tephrosia vogelii). Kuna aina kuu tatu za Utupa ambazo hutofautiana kwa maua yake, yaani; Njano, Pinki na Nyeupe. Ni mmea unaositawi zaidi kwenye ukanda wa nyanda za juu, mmea huu si rafiki wa ukame. Huchukua miezi 3 hadi 5 tangu kupandwa kuanza kutumika. Huweza kudumu hadi zaidi ya miaka mitatu. Sehemu zenye madhara ni Majani na Mizizi. Majani machanga ambayo hayajakomaa ndiyo yenye kiwango kingi cha sumu. Unashauriwa kuukata miti ya Utupa inapofikia miaka mitatu ili ichipue upya, hii husaidia kurefusha muda wa kuishi kwa mmea huu.

MATUMIZI YA UTUPA.

(i) Kufukuza Panya/ Mchwa.

Mti huu husaidia kuondoa wadudu na wanyama waharibifu wanaokaa ardhini. Panda Utupa 3m kila upande (3m * 3m) na mpakani mwa shamba lako, baada ya mwaka mmoja shamba lako litakuwa halina mashimo ya Panya. Kama kichuguu cha Mchwa panda mmea huu karibu na kichuguu na baada ya mud kitakufa.

(ii) Kuogesha Mifugo

Chukua kilo 1 ya majani ya Utupa na Maji lita 25, loweka kwa masaa 4 hadi 6 au chemsha kwa dakika 30 na lita 27 za maji, chuja kwa kitambaa, kisha osha mifugo yako.
Changanya na sabuni ya unga kidogo dawa iweze kunata na kukaa kwenye ngozi ya mnyama.
ONYO: Usitumie majani ya Utupa kuogeshea Nguruwe, hawana uwezo wa kuhimili dawa hii kwenye ngozi zao.

(iii) Kunyunyizia shambani.

Chukua kilo 1 ya Majani ya Utupa na maji lita 5, loweka kwa masaa 10 hadi 16 kisha chuja na weka kwenye bomba, tayari kwa kupulizia shambani. Ina uwezo wa kuua aina ya wadudu wote shambani.

(iv) Kuhifadhi Nafaka ghalani.

Pima gramu 100 za unga wa majani ya Utupa, changanya na Mahindi au Maharage kilo 100. Dawa hii huwa na nguvu kwa muda wa mwaka mzima.

Kwa wale wenye mashamba ya kahawa ni vema na muhimu sana kupanda Utupa kuzunguka mashamba yenu na kama shamba ni kubwa sana unaweza panda na katikati ya shamba pia. Faida nyingine ya mmea huu, hurutubisha udongo maana ni jamii ya mikunde.

Ndugu zangu wakulima, nawashauri muanze sasa kupanda Utupa shambani na nyumbani pia.

Ahsanteni!
Happy New Year.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete