Saturday, January 18, 2014

Kuku wa asili pia wanahitaji viinilishe vyote muhimu kama ilivyo kwa kuku wa kigeni kama wale wa nyama na mayai. Swala la msingi katika lishe yao ni kuzingatia gharama ya uzalishaji kama inampatia mfugaji faida.

Walishwe chakula chenye mchanganyiko wenye virutubisho vyote muhimu ambavyo ni:-

(i) Vyenye asili ya wanga mfano mahindi, pumba, mtama n.k
(ii) Vyenye asili ya protini mfano dagaa, soya, mashudu, damu n.k
(iii) Vyenye asili ya madini mfano mifupa iliyosagwa, chokaa, premix ya kuku n.k
(iv) Vyenye asili ya vitamini mfano mboga mboga, vitamini maalumu zinazopatikana madukani.

Kiwango cha kila kiinilishe ni lazima kizingatiwe ili kuku aweze kupata uwiano sawa wa viinilishe swala ambalo ni muhimu katika uzalishaji wake. Michanganyiko hii inaweza kutumika ama kuboresha kulingana na upatikanaji wa vyakula hivyo.

Katika kutengeneza chakula cha kuku mfugaji lazima kwanza azingatie kiasi cha protini na wanga na uwiano wake. Protini inayotolewa lazima izingatie ubora wake katika viasili hivi yaani LYSINE, METHIONINE na CYSTINE. Pia chakula lazima kizingatie kiwango cha madini hasa CALCIUM na PHOSPHORUS na mahitaji ya vitamin. Baada ya kujua haya mfugaji anaweza kutengeneza chakula chake mwenyewe. Kiwango cha vitamini D ni muhimu sana kwa matumizi ya madini ya calcium na phosphorus.

Uchanganyaji wa chakula cha kuku kwa makundi yote:

Protini 25%
Mimea 18-22%
Wanyama 5-8%

Wanga 68%
Pumba za mahindi 60-68%

Madini 7%
Calcite 5%
Madini maalumu (standard mineral mixture) 2-3%

Vitamini (premix)- hii inategemea maelekezo ya mtengenezaji.

Hebu tuangalie sasa uwiano wa uchanganyaji:

- Pumba za mahindi 66kg
- Mashudu ya alizeti 18kg
- Dagaa 7kg au (4kg Dagaa 3 Damu), 4 dagaa 3 soya)
- Mifupa iliyosagwa 5kg
- Chokaa 2kg
- Madini/vitamini maalumu 2kg

Jumla ya mchanganyiko ni 100kg kwa uwiano.

Lakini pamoja na ulishaji huo kwa kuku, mfugaji hana budi kufuata na kutekeleza ratiba ya kuzuia magonjwa (Chanjo) na kutoa tiba sahihi ugonjwa unapotokea.

Ahsanteni!
HAPPY NEW YEAR!

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete