Saturday, January 25, 2014

Kwa leo ndugu wasomaji nitayaelezea magonjwa mawili yasiyo na tiba ya kuku. Ili mkulima uweze kutambua jinsi ya kuwakinga kuku wako na kuepusha vifo vya kuku vinavyoweza kutokea kwa kutofuata taratibu za uchanjaji na kinga kwa ujumla.

1. Ugonjwa wa Mdondo (Newcastle Disease)

Ugonjwa huu husababishwa na virusi, huathiri mifumo ya fahamu, chakula na upumuaji. Mara nyingi huwapata kuku wakubwa wa umri miezi 5-8.

Dalili za ugonjwa
- Vifo vingi vya ghafla.

- Mharo wa kijani na wakati mwingine ukiwa na damu.

- Macho na koo hujaa maji.

- Kunyonga shingo.

TIBA: Ugonjwa huu hauna tiba.

KINGA: Chanja siku ya kwanza hadi ya tatu baada ya kuanguliwa kisha na urudie kuwachanja baada ya wiki 3-4. baada ya hapo, kila baada ya miezi 3.
Zuia uingiaji wa watu, kuku, wageni au vifaa kwenye banda hasa toka kwenye maeneo yenye maambukizo.
Wapewe antibiotics i.e Doxycol, Fluban, OTC 20% na Vitastress na Amprolium kuzuia magonjwa nyemelezi.

2. Ndui ya kuku (Fowl Pox)

Ugonjwa huu unasababishwa na kirusi ambaye huenea taratibu na kusababisha upele kwenye kishungi, ngozi na mfumo wa hewa. Huwapata kuku wa umri mbalimbali.

DALILI

- Upele kwenye ngozi ya shingo na maeneo mengine yasiyo na manyoya kama miguu, na sehemu ya kutolea kinyesi.

- Vipele hupasuka na kufanya gamba gumu (scab)

- Utando mdomoni/puani unaoambatana na mafuta.

- Vipele vya puani humfanya kutoka majimaji puani.

- Vipele vya machoni husababisha kutoka kwa machozi.

- Maambukizi ni ya taratibu lakini vifo hutokea hadi 50%.

TIBA

Ugonjwa huu hauna tiba. Kuku wapewe vitamin ili kuwaongezea hamu ya kula. Kuku wapewe viuavijasumu (antibiotics) i.e OTC 20% kuzuia magonjwa nyemelezi.

KUZUIA

Kuku wapatiwe chanjo ya ndui. Chanjo hutolewa kwenye maji ya kunywa ama kuchomwa sindano kwenye bawa.

CHANJO

Chanjo itolewe mara mbili kama ifuatavyo:-
(i) Kati ya siku 5-26 (wastani wa umri wa wiki 4)
(ii) Chanjo ya pili itolewe mwezi (1-2) kabla ya kuku kuanza kutaga.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete