Tuesday, March 15, 2016

Habarini ndugu zangu wapenzi wasomaji wa mtandao wangu, poleni na shughuri za ujenzi wa taifa.   Hatukuwa pamoja kwa wiki kadhaa kutokana na majukumu mbali mbali.

Mhogo ni zao linalookoa jamii nyingi hapa nchini hasa inapotokea ukame. Linahimili ukame na pia hutumika kuandaa bidhaa zingine ambazo zinatokana na nafaka kama vile Unga, chips , keki na Maandazi.

Tanzania ni nchi ya nne kwa uzalishaji wa muhogo barani Afrika, ambapo inakadiriwa huzalisha takribani tani milioni 5 Kwa mwaka ikiwa ni wastani wa tani 8 kwa hekta.
Karibu hekta 670,000 za ardhi ya kilimo zinatumika kuzalisha Muhogo. Muhogo ni zao muhimu la chakula baada ya Mahindi. Linachangia Karibu 15% za chakula nchi nzima.
Inakadiriwa zaidi ya kaya 1.3 milioni zinajishughulisha na kilimo cha Muhogo nchini hasa mikoa ya Pwani na kanda ya Ziwa.

Kuanzia miaka ya katikati ya 90 zao hili lilianza kupotea kutokana na kuingia ugonjwa wa Batobato na Mnyauko. Wataalamu walihangaika kukabiliana na magonjwa haya bila mafanikio.

Njia rahisi ya kukabiliana na magonjwa haya ni kuruhusiwa kutumika kwa technologia ya GMO, Genetic Modified Organisms. Kutokana na technologia ya GMO, watafiti kutoka katika kituo cha utafiti cha Nliendele huko Mtwara chini ya Dr. Godfrey Mkamilo, wamefanikisha kupatikana kwa mbegu bora ya Muhogo aina ya KIROBA ambayo haiathiriwi na magonjwa haya hatari. Mbegu ameshafanyiwa utafiti na majaribio ya kutosha na wakulima hasa wa mikoa ya Lindi na Mtwara wameikubali na kuipenda sana maana inazaa sana, mikubwa mikubwa na siyo michungu.
Mbegu hii huzaa tani 25-30 kwa hekta na huvunwa kuanzia miezi 9 toka ipandwe.

Zao la muhogo likiimarishwa vizuri litasaidia kuimarisha usalama wa chakula hasa maeneo ya ukame nchini.

Note:
          Kuna kemikali iitwayo Cynogenic Glucoside ambayo inaweza kuwa sumu endapo mihogo haitaandaliwa vizuri. Kiwango cha sumu hii ni kikubwa kwenye mihogo michungu.

Imetayarishwa na kuandikwa na
Marcodenis E. Misungwi.
Agriculture Extensionist.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete