Wednesday, November 11, 2015

On 11 Nov 2015 08:33, "Marcodenis Misungwi" <mmisungwi@gmail.com> wrote:

Habari ndugu mpenzi msomaji wa makala zangu za kilimo na mifugo Katika blog yangu hii. Nakukaribisha tena tujifunze pamoja.
Kwanza nitangulize samahani sana kwa kosa la kimtandao lililojitokeza ambapo ilijikuta baadhi ya makala karibu 25 kufutika kwenye mfumo wa kuonekana moja kwa moja. Pole kwa hilo.

Najua kwa nyakati za sasa watu wengi wamejikita katika kufuga kuku wa kisasa kibiashara, wanaweza kuwa wa Mayai ama wa Nyama.
Leo basi tuangalie matunzo yake kuanzia siku ya kwanza unapowachukua mpaka siku ya 90 au miezi 3.

1. Utayarishaji wa banda.

i. Banda liwe safi, lisafishwe lisiwe na vumbi.

ii. Pulizia dawa ya kuondoa viroboto, utitiri na chawa kwa kutumia dawa kama Ectomin Dip.

ii. Pulizia dawa ya kudhibiti wadudu wasababishao magonjwa, tumia disinfectant mfano Vivid/TH4.

Tayarisha taa na moto (charcoal) kwa ajili ya kuweka chumba kiwe na joto la kutosha.

SIKU YA 1.
                 i.  Vifaranga wanapofika tu wapewe Glucose kwenye maji kwa masaa 8 mfululizo.

                ii. Baada ya hapo wapewe Vitalyte kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 3.
                 Wapewe chanjo ya Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Vitalyte au Antistress kwa siku 3 mfululizo.
               
SIKU YA 7.
                Wapewe chanjo ya Gumboro Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie maji ya Antistress kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 10.
                   Wapatie OTC Plus kwa siku kwa saa 24 kwa siku 3 mfululizo.

SIKU YA 14/18/19.
                  Wapatie Esb3 na Vitalyte kwa masaa 24 kwa siku 3 mfululizo.

SIKU YA 21.
                  Wanyweshe Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Antistress kwa siku 4 mfululizo.

SIKU YA 28.
                 Wapewe Gumboro Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Antistress kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 31.
                  Wapatie  OTC Plus kwa siku 7 mfululizo.

SIKU YA 43/44/45.
                  Wapatie Esb3  na Vitalyte kwa masaa 24 mfululizo kwa siku 3.

SIKU YA 50.
                 Wapewe chanjo ya Fowl Pox. Baada ya hapo endelea kuwapa Chickmycin au Chick Plus kwa wiki 2 mfululizo.

SIKU YA 65.
                  Chanjo ya Gumboro na baada ya hapo endelea na Antistress.

SIKU YA 69.
                  Wapatie dawa ya Minyoo mfano Levalap kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 72.
                 Wapewe Fluquin kwa siku 5 mfululizo.

SIKU YA 79.
                 Wapewe Anticox na Vitalyte kwa siku 5 mfululizo.

SIKU YA 90.
                  Wapewe tena chanjo ya Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo.
Baada ya hapo endelea kuwapa Antistress kwa siku 3 mfululizo.

Hapo sasa endelea na Utaratibu wa kawaida wa chanjo na tiba.

     Prepared by
         Marcodenis E. Misungwi.

1 comments:

  1. CONTACT: onlineghosthacker247 @gmail. com
    -Find Out If Your Husband/Wife or Boyfriend/Girlfriend Is Cheating On You
    -Let them Help You Hack Any Website Or Database
    -Hack Into Any University Portal; To Change Your Grades Or Upgrade Any Personal Information/Examination Questions
    -Hack Email; Mobile Phones; Whatsapp; Text Messages; Call Logs; Facebook And Other Social Media Accounts
    -And All Related Services
    - let them help you in recovery any lost fund scam from you
    onlineghosthacker Will Get The Job Done For You
    onlineghosthacker247 @gmail. com
    TESTED AND TRUSTED!

    ReplyDelete