Sunday, December 29, 2013

WALAJI WA NYAMA YA NGURUWE HATARINI KUUGUA KIFAFA.

Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Kimehadhalisha walaji wa nyama ya Nguruwe nchini kuwa wanakabiliwa na hatari ya kupata kifafa. Utafiti wa kisayansi uliofanywa na SUA umebaini kuwa baadhi ya Nguruwe wana minyoo aina ya Tegu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri, mlaji atapata minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na kusababisha kifafa.

Mhadhiri na Mtafiti Idara ya sayansi ya Wanyama na Uzalisha ya SUA, Profesa Faustine Lekule, alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya zimebaini Nguruwe wakiwamo wanaosafirishwa katika miji mikubwa wameathirika na minyoo hiyo.

Kwa mujibu wa Prof. Lekule, wataalamu wa SUA wanaosimamia mradi wa utafiti wa kuboresha ufugaji wa Nguruwe kwa mkoa wa Mbeya ili kuinua pato la kaya, unaofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Denmark (DANIDA), walibaini hatari hiyo baada ya kuchukua sampuli ya nyama ya Nguruwe kwa ajili ya vipimo. "Majibu ya Sampuli ambazo wataalamu wamezichukua kutoka kwa Nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji, wamebainika kukumbwa na hatari hii. Lazima jitihada za makusudi zichukuliwe katika kutafuta ufumbuzi wa pamoja wa tatizo hili kati ya watafiti na serikali" alisema Profesa Lekule.

Alisema maambukizi ya tegu au minyoo ya Nguruwe yanatokana na tabia za baadhi ya wafugaji kutozingatia ufugaji bora kwa kuwaacha Nguruwe kujitafutia chakula na maji mitaana na kula kinyesi cha binadamu.

Kwa mujibu wa Prof. Lekule, baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwaacha Nguruwe kutafuta malisho ktk vichaka na kula kinyesi chao, hali inayochangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya tegu hao. Baada ya kula kinyesi minyoo humwingia mwilini na kumdhoofisha na baadaye binadamu anapokula nyama ambayo haijaiva vizuri minyoo hiyo humwingia na kusababisha kifafa baada ya kuingia kichwani.
Alisema athari za kuenea kwa maambukizi hayo inaweza kutokea ktk miji mikubwa ikiwamo Dar es salaam kwa kuwa nguruwe wa Mbeya husafirishwa na kuuzwa maeneo hayo. "Hatua hii inaweza kusababisha kusambaa kwa ugonjwa huu" alisema Profesa Lekule.

Thursday, December 26, 2013

SHAMBANI SOLUTIONS: TANZANIA TO HOST AGRIBUSINESS EVENT WHICH WILL SHO...

SHAMBANI SOLUTIONS: TANZANIA TO HOST AGRIBUSINESS EVENT WHICH WILL SHO...: Agribusiness Congress East Africa programme director Amore Swart said that interest in the conference had "surpassed expectations&qu...

Wednesday, December 25, 2013

KRISMASI NI SHEREHE ZA KIDINI?

HISTORIA YA KRISMASI

Ndugu zangu leo ni Krismas, ni sherehe zinazoazimishwa kila mwaka tarehe kama ya leo mwezi kama huu 25  Desemba. Sherehe hizi ni za kuazimisha kuzaliwa kwa Yesu Kristu kama inavyojulikana. Sherehe hizi zinaazimishwa na Wakristu karibu wote duniani isipokuwa Waadventista Wasabato ambao wanaamini katika Biblia. Hebu tujiulize je sherehe hizi ni za kidini au zimeanzishwa na binadamu?

  Wakati wa zama za kale , siku ya mwisho ya majira ya baridi huko sehemu za kusini kulisheherekewa mfano wa usiku ambao mungu wa mama watakatifu alijifungua mtoto akijulikana kuwa ni Mungu wa jua.Pia siku hii inaitwa Yule, siku ambayo inasheherekewa  mno kwa kurushwa pashpashi. Ambapo kila mtu atacheza na kuimba ili kuliamsha jua kutokana na usingizi wake mnono wa majira baridi.

Wakati wa Warumi, iliazimishwa kwa kumsifu Satanusi (mungu wa mavuno) na Mithrasi (mungu wa kale wa nuru), huo ni mtindo wa kuabudia jua ambao umekuja ukitokea Syria hadi Urumi Karne kabla ya madhehebu ya Sol Invictus, ilitangaza ya kwamba, majira hayo ya baridi sio ya milele, na kwamba maisha yanasonga mbele, na ni mwaliko wa kubaki kwenye nguvu nzuri.

  Siku ya mwisho ya majira ya baridi  huko sehemu za mviringo za kusini ni baina ya siku ya 20 au 22 Disemba. Warumi waliadhimisha Saturnalia baina ya tarehe 17 na 24 Disemba.

Wakristu wa kale

Ili kuepuka kuchunguzwa wakati wa sherehe ambazo ni za wapagani, Wakristu wa kale walikaa majumbani  mwao pamoja na mtakatifu Saturnalia. Kwa vile idadi ya wakristu iliongezeka na mila zao zikaenea, sherehe zikachukua shurti za kikristu. Lakini makanisa ya kale hakika hayakusheherekea mwezi Disemba kwa kuzaliwa Kristu hadi alipokuja Telesforusi ambaye alikuwa askofu wa pili wa Roma kutoka mwaka 125 hadi 136, askofu huyo ndiye aliyetangaza  kwamba huduma za Kanisa zifanywe wakati huu ili kuadhimisha "kuzaliwa kwa Bwana wetu wa Mwokozi". Hata hivyo kwa vile hakuna mtu  hata mmoja aliye na uhakika wa mwezi ambao amezaliwa Kristo,  kawaida ya Uzawa  ulikumbukwa Septemba, ambao ulikuwa ni wakati wa sherehe za Kiyahudi za Trumpetse (kwa sasa ni Rosh Hashanah). Ukweli ni kuwa, kwa zaidi ya miaka 300,  watu waliewa kuzaliwa kwa Yesu katika tarehe tofauti.

  Katika mwaka 274, kikomo cha jua kiliangukia tarehe 25 Disemba. Mfalme wa Roma aitwye Aurelian alitangaza tarehe hiyo kama ni "Natalis Solis Invict", 'Sherehe ya kuzaliwa Jua lisiloshindikana'.
Katika mwaka 320, Papa Julius I aliitangaza tarehe 25 Disemba kama ni tarehe rasmi ya kuzaliwa Yesu Kristu.

  Mnamo mwaka 325, Krismasi ilitangazwa rasmi, lakini kiujumla haikutiliwa  maanani. Mtakatifu Constatine, ambaye ni mfalme wa mwanzo wa dhehebu la ukristu la kirumi, aliitanguliza Krismasi kama ni sherehe isiohamishika  kwa tarehe 25 Disemba. Pia aliitanguliza  Jumapili kama ni siku kuu ndani ya siku saba za wiki, na aliitanguliza  Pasaka kama ni sherehe yenye kuhamishika. Mnamo mwaka 354, Askofu Liberius wa Rumi, alitoa amri rasmi kwa wafuasi wake kusheherekea kuzaliwa kwa Yesu ndani ya tarehe 25 Disemba.

  Hata hivyo, ingawa, Costantine aliifanya rasmi tarehe 25 Disemba kama ni sherehe ya kuzaliwa Kristo, Wakristo wakiitmbua kama ni tarehe ya sherehe iliyofanana na mapagani, hawakushiriki katika mambo mazuri (kwa siku hii) iliyopangwa na Askofu. Krismasi ilishindwa kupata utambulisho wa kilimwengu miongoni mwa wakristo hadi kipindi cha hivi karibuni.
Hata hivyo bado krismasi haikuwa ni sikukuu halali hadi miaka ya 1800.

Krismasi inaanza kuwa maarufu

Umaarufu wa krismasi ulianza ghafla mnamo mwaka 1820, ulianza ghafla mnamo mwaka 1820. Ilikuja kuwa maarufu ni maarufu mno hadi kufikia kwamba sio makanisa wala serikali kukana umuhimu wa sherehe za krismasi. Mnamo mwaka 1836, Alabama ilikuja kuwa ni taifa la kwanza ndani ya marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mwaka 1907, Oklahoma ilikuwa ni ya mwisho miongoni mwa mataifa ya Marekani kutangaza Krismasi kama sikukuu halali. Mwaka baada ya mwaka nchi za dunia nzima zilianza kuitambua Krismasi kama ni siku ya kusherehekea kuzaliwa kwaYesu.

Leo, mambo mengi yasiyokuwa ya kikristu yananasibiwa ndani ya Krisimasi. Kulingana na nyakati katika Biblia, Yesu alizaliwa mwezi Machi, bado yake ya kuzaliwa inasheherekewa Disemba 25. Sherehe za Krismasi zinamalizikia siku kumi na mbili za krismasi (Disemba 25 hadi Januari 6), ni idadi hiyo hiyo ya siku ambazo zilisheherekewa na wapagani wa ki-rumi wa kale kwa kuadhimisha kurudi kwa Jua.

Je, Krismasi ina ushahidi wa ki-biblia?

Neno 'Krismasi' halipo ndani ya Biblia. Biblia ilifunga midomo ya sherehe yote inayohusiana na Krismasi, isipokuwa kwa kwa kimoja; upambaji wa mti. Biblia yenyewe inashutumu upambaji wa mti (ya krismasi):  "Mila za watu si chochote, wanakata mti kutokana na msitu, na mchongaji anauchonga kwa patasi yake, wanaupamba kwa fedha na dhahabu, wanaunganisha kwa nyundo na misumari ili usipate kutikisika" (Jeremia 10-3,4).

Ndugu zangu, tunapoendelea kusheherekea Krismasi, tujiulize swali hilo la 'Je, Krisimasi ni sherehe za kidini?'   Ahsanteni sana na Sikukuu Njema.

Sunday, December 22, 2013

KANUNI ZA KILIMO BORA CHA MAHINDI.

                                       





KANUNI YA KWANZA

Panda mapema

Tayarisha shamba mapema kwa zana yoyote iliyo ndani ya uwezo wako (jembe, maksai, trekta).
Kwa wilaya ya Mbozi Panda kuanzia tarehe 15 Novemba hadi kati kati ya mwezi Desemba.

KANUNI YA PILI

Panda kwa nafasi

Mmea hadi mmea: sentimeta 30 (sawa futi moja). Weka mbegu moja kila shimo au sentimeta 60 (futi 2). Weka mbegu mbili kila  shimo.

Mstari hadi mstari: sentimeta 75 (au futi 2 na nusu). K wa wanaopenda kufuata mfereji
 wa jembe la maksai inapendekezwa nafasi iwe sentimeta 90 na mbegu zidondoshwe sentimeta 25.

Usipokuwa na uhakika wa uotaji panda mbegu 2 au 3 kwa kila shimo. Yakiota yote punguza yabaki moja (au mawili) kila shimo kwa kusokota mhindi na kuvuta ili mzizi wa mmea unaobaki usidhurike.

KANUNI YA TATU

Panda mbegu bora: Kuna aina tatu za mbegu, chotara (hybrid), kompositi na kienyeji (asili).

Sehemu za miinuko ya juu (mita 1500-2300 kutoka usawa wa bahari), UH615, UH6303, TMV-2, PAN691, H625, H614D, Seedco627 nk.

Sehemu za miinuko ya kati (100-1500) UH6303, TMV-2, SC627, Staha, Kilima nk.
 Nunua kilo 10 kwa kila eka, mbegu zinazobaki zitumie kurudishia ambazo hazitaota/kuharibiwa na ndege au Panya.

Nunua mbegu bora kwenye mifuko yake halisi. Pia dai risti ili uweze kuhalalisha malalamiko endapo mbegu hiyo itakuwa na matatizo baadaye. 

KANUNI YA NNE

Tumia mbolea.

Samadi/mboji: Tani 5-8 kwa ekari.

Changanya na mfuko 1 wa TSP kwa ekari. Weka mbolea kwenye shimo la kupandia au rutubisha shamba zima kwa kuifukia kwa jembe la mkono, maksai au trekta kabla ya kupanda.

Mbolea za chumvi chumvi.  
Mtiririko huu unaonyesha matumizi ya Nitrogen inayohitajika wakati wa kupanda na wakati wa kukuzia.

Sehemu zenye mvua nyingi (mm 750 au zaidi)
-SA mfuko 1 na nusu kupandia, mifuko 3 kukuzia.
-CAN mfuko 1 kupandia, mifuko 2 na nusu kukuzia.
-UREA mfuko 1  kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-DAP mfuko 1 kupandia, SA 4, au CAN 3 au Urea 2 kukuzia.

Maeneo yenye mvua haba (mm550-750)
-SA 1 kupandia, mifuko 2 kukuzia.
-CAN 1 kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-UREA nusu mfuko kupandia, mfuko 1 na nusu kukuzia.
-DAP 1 kupandia, SA 4 NA nusu au CAN 3 au Urea 1 kukuzia.

Katika maeneo yenye mvua chini ya mm 550 kwa msimu ni lazima umwagiliaji ufanyike.

KANUNI YA TANO

Palilia vizuri.

Palilia mahindi mara 2 au 3, palizi ya kwanza iwe wiki 2-3 baada ya mbegu kuchipua. Ya pili au tatu baada ya mbegu kuchanua. Uzaaji hauongezeki ukipalilia baada ya mhindi kuchanua. Kwa wenye uwezo zipo dawa za kuua magugu (mfano PRIMAGRAM, ATRANEX, GESAPRIM, GRAMAXONE, ROUNDUP nk)

KANUNI YA SITA

Zuia wadudu waharibifu (hasa bungua)

Nyunyizia dawa kwenye majani ya mahindi yakiwa na urefu wa sm75, rudia baadae ukiona mashambulizi.

Dawa za viwandani: Actellic, Thionex, Endosulfan, Dursban, Karate, Dimepaz 40 na nyinginezo.Kipimo: mls 30 kwa lita 15 za maji.

Dawa za asili: kwa mfano utupa, dawa hizi hazina kiwango maalumu.

NB: Mbegu bora za mahindi zina uwezo wa kustahimili magonjwa ya mahindi.

KANUNI YA SABA

Hifadhi vizuri kwenye mifuko, ghalani au mapipa.

Hakikisha sehemu hizo ni kavu, safi, dawa za kuua wadudu zimepulizwa maeneo hayo. Actellic EC 50 ya maji inafaa sana kudhibiti wadudu wa ghalani.

Mkulima, zingatia kanuni za uzalishaji bora wa Mahindi ili kuongeza kipato.
 

Saturday, December 21, 2013

KILIMO CHA MAPARACHICHI KIBIASHARA.

Matunda ya Maparachichi yanazidi kuwa ni mazao ya muhimu katika nchi za joto na joto kiasi katika ulimwengu. Kutokana na taarifa ya mwaka 1976, nchi ya Mexico ndiyo inayozalisha kwa wingi duniani ikifuatiwa na Marekani na Brazil.

UZALISHAJI KATIKA AFRIKA.

Maparachichi, mara nyingi hupandwa mbegu zake, huzalishwa kwa ajili ya chakula cha nyumbani katika maeneo mengi Afrika. Hata hivyo ni nchi chache zimeweza kuendeleza uzalishaji kwa kiasi kikubwa kwa ajili ya uuzaji nchi za nje. Kwa sasa Maparachichi husafirishwa na kuuzwa ulaya kutoka Ivory Coast, Cameroon, Kenya, Swaziland na maeneo mengine ya kusini mwa Africa.

Maparachichi hustawi vizuri katika hali ya joto. Mimea ya Maparachichi hupandwa umbali wa mita 8 kwa mita 1. Katika eka moja kunaweza kukawa na idadi ya miti chini ya 400.

BIASHARA.

Kama kila mti utazaa matunda 50 kwa kiwango cha chini, kwa hiyo miti 400 itazaa matunda 400 * 50= 20,000. Ikiwa kila tunda litauzwa kwa shilingi 200 bei ya jumla, fedha itakayopatikana ni sh 20,000 *200 = 4,000,000/= zingatia kwamba hilo zao utavuna kwa muda mrefu sana.
Unaweza kununua miti ya Maparachichi iliyofanyiwa budding tayari na kupanda shambani kwako. Katika muda wa miaka mitatu utaanza kuvuna matunda.

Kwa nini Tanzania hatumo kwenye orodha ya nchi zinazozalisha Maparachichi wakati tuna eneo kubwa na hali ya hewa inayoruhusu karibu katika kila mkoa nchini kwetu? Ni jambo la aibu na fedheha kubwa kuona tuko nyuma kwa kila jambo. Wakulima sasa hebu tuamke na tuangalie fursa zingine ndani ya kilimo chetu.

Kuna mazao mengi sana ambayo kama mtu atajikita katika kuyafanyia kazi, mafanikio ya uhakika yatakuwepo. Kwa mfano kuna Miwa. Lima ekari moja ya miwa, ekari moja unaweza ukavuna miwa 100,000. Na kama utauza kila muwa kwa jumla Tshs. 300 utaweza kupata Tshs. 30,000,000/= hicho ni kiwango cha chini kabisa. Fikiria una ekari 10.

Kwa hiyo ndugu mkulima, hebu jaribu kuwaza zaidi ya hapo ulipo ili uweze kuona thamani ya kilimo. Tuondoe ile dhana ya kwamba kulima ni shida au mazoea.
KILIMO NI BIASHARA.


Ahsanteni 

Prepared by:

Marcodenis E. Misungwi 

Agriculture Field Extension Officer. 

Thursday, December 19, 2013

LINI MAHAFALI YA MKULIMA MDOGO MDOGO YATAFIKA?

Habari ya siku mbili tatu ndugu zangu wakulima, ni kama siku tano sasa sijawawekea chochote humu. Ni majukumu tu yalinizidi wakulima wenzagu.
Leo hii nataka niwashirikishe jambo moja, na jambo hili inabidi kila mmoja wetu ajiulize swali hili "Je, Mahafali ya Mkulima Mdogo Mdogo ni Lini?" Kila mkulima ajiulize yeye ni mkulima wa aina gani, je ni mdogo, ni wa kati au ni mkubwa? Kama ni wa kati, je umesheherekea mahafali ya kuhitimu na kuwa mkulima mkubwa?

Leo hebu tumjadili huyu mkulima mdogo, ambaye ndiye anayechukua asilimia kubwa ya wakulima wa nchi yetu Tanzania, ambaye ndiye aliye kwenye sekta inayoajiri watu wengi kuliko sekta zote nchini, zaidi ya 75%.

Mkulima huyu tangu enzi anaitwa mkulima mdogo mdogo, viongozi wa serikali na wanasiasa wanaimba kila siku "kumsaidia mkulima mdogo mdogo". Sasa basi tuangalie huyu mkulima mdogo mdogo (small holder farmer) anafanya yeye kama yeye na anawezeshwa kwa dhati kwamba atoke alipo? Au amewekwa kama daraja la kuvukia kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine kwa manufaa ya vitu vingine tofauti na yeye?

Leo hebu tuangalie sehemu moja, Serikali, katika kumsaidia huyu Mkulima Mdogo (small holder farmer) ili aweze kutoka hapo alipo na apande daraja lingine la juu zaidi.
Ni kweli serikali ina jukumu la kuajiri mabwana shamba ambao ndio wanafanya kazi karibu kabisa na Mkulima huyu, lakini huyu Bwana Shamba anaifanya kazi kwa dhati na moyo mmoja? Je, amepewa vitendea kazi? Jibu sahihi ni kweli kuna ambao ni mzigo kwa Mkulima, lakini wapo wanaoifanya kazi yao kwa moyo mmoja na bidii zote kakini wanakwamishwa na ukosefu wa vitendea kazi.

Serikali ndie mhimili wa kila kitu ktk nchi. Kuna Msaada serikali iliupokea kutoka Japani wa mbole ya kupandia aina ya DAP tani 6003.8, ikimulenga mkulima mdogo mdogo, cha kushangaza anayelengwa hajaambiwa, haijatangazwa utaratibu wake, imeonekana sokoni tu ikiuzwa, ambapo inawezekana mlengwa isimfikie maana hajui chochote. Picha hapo juu inamuonyesha waziri wa kilimo akizipokea!

Tujiulize, huyu mkulima atahitimu lini?

Friday, December 13, 2013

SHAMBANI SOLUTIONS: A BILLIONAIRE'S ADVICE: "INVEST IN AGRICULTURE"

SHAMBANI SOLUTIONS: A BILLIONAIRE'S ADVICE: "INVEST IN AGRICULTURE": Bilionare Jim Rodgers  That pearl of advice is from Jim Rogers, the Demopolis, Ala., native who began his business career selling...

Tuesday, December 10, 2013

UTAYARISHAJI WA MBOGA ZA MAJANI

  Mboga za majani zinashika nafasi muhimu sana katika vyakula vyetu.
 Zinaliwa kila na mara nyingi zaidi ya mara moja kwa siku. Zipo aina nyingi za mboga za majani , zingine zinalimwa na zingine zinaota zenyewe porini na mashambani wakati wa msimu wa mvua. Mboga zina virutubisho kama madini na vitamini ambavyo vinahitajika mwilini kwa afya bora. Hata hivyo pamoja na kwamba vina virutubisho vya kutosha, na zinaliwa kila siku, watu wengi wanapata matatizo ya afya yanayotokana na ukosefu wa virutubishi vinanyotokana katika mboga za majani kwa mfano upofu na upungufu wa damu.

Hali hii inajitokeza kwa sababu gani?

  Mojawapo ya sababu ya kuvikosa virutubishi ni utayarishaji usiokuwa mzuri wa mboga za majani kabla ya kula. Utayarishaji wa mboga hizi ni shughuli zote zinazohusiana na kuandaa, kupika na kuweka tayari kwa kula. Wakati wa utayarishaji virutubishi muhimu vinaweza kupotea kama mambo muhimu hayazingatiwi. Kupika ni muhimu kwa sababu kuna faida zifuatazo;

             FAIDA ZA KUPIKA

- Kupika kunaua vijidudu vibaya viletavyo magonjwa kwenye chakula.
- Kunaua vimeng'enyo vilivyomo ndani ya chakula ambavyo vinaweza kuharibu chakula.
- Kubadili rangi na kuboresha radha ya chakula.
- Kuboresha uyeyushaji wa chakula mwilini.

  Pamoja na faida hizi, kupika chakula pia kunaweza kuleta upotevu wa virutubishi muhimu iwapo hautafanyika vizuri.

            DOSARI ZA UTAYARISHAJI

- Mboga nyingi huchambuliwa na kukatwakatwa vipande vidogo ndipo zinaoshwa.
- Mboga hubandikwa jikoni na maji baridi.
- Baadhi ya mboga huchemshwa na maji mengi halafu maji yanayochemshia humwagwa.
- Kama mboga ni kavu zinalowekwa kwenye maji halafuayale maji yanamwagwa.
- Mboga inapikwa kwa muda mrefu sana zaida ya nusu saa na mara nyingine bila kufunikwa.
- Mara nyingine mboga haziliwi mara tu baada ya kutayarishwa.

            KWA NINI UTAYARISHAJI WA NAMNA HII HAUFAI.

  Upishi wa namna hii unasababisha upotevu wa virutubisho muhimu kama vitamini C, A na vitamini B1, vitamini hizi muhimu zinayeyuka kwenye maji kwa urahisi, kwa unapokatakata vipande vidogo vidogo na kuosha kwa kiasi kikubwa zinapotea kwenye maji uliyotumia kuoshea au kupikia iwapo maji hayo yanamwagwa na hivyo virutubisho hivi muhimu hupotea. Mboga zioshwe kwanza kabla ya kukatakata.

           VITAMINI C HUPOTEA PIA IKIWA;

- Mboga zinatayarishwa halafu zinaachwa kwa muda mrefu kabla ya kupikwa.
- Mboga zinapikwa na kuachwa kwa muda mrefu kabla ya kuliwa.
- Mboga zinapoa halafu zinapashwa moto kabla ya kuliwa.

            VITAMINI A HUPOTEA WAKATI WA KUTAYARISHA MBOGA KAMA;

- Mboga inachemshwa kwa muda mrefu bila kufunikwa.
- Mboga inakaangwa kwenye mafuta yenye joto kali kwa muda mrefu.

             MADINI MUHIMU HUPOTEA IKIWA;

- Maji yanayochemshia mboga humwagwa.

      Mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa utayarishaji wa mboga za majani.

- Chagua mboga nzuri ambazo hazijasinyaa au kuanza kuoza.
- Zingatia usafi wakati wa kupika kama ifuatavyo;
                   * Tumia maji safi
                   * Mahali pa kupikia pawe safi
                   * Vyombo vyote vinavyotumika viwe safi
                   * Nawa mikono na sabuni kabla ya kuanza kupika na uwe msafi
- Osha mboga kwa maji safi kabla ya kukatakata
- Loweka mboga kavu kwenye maji ya kutosha tu kuzifunika na tumia maji hayo wakati wa kupika mboga hiyo.
-Kama mboga ni za kuchemsha, chemsha mboga kwenye maji kidogo yanayochemka ya kutosha kuivisha mboga. Usimwage maji ambayo umetumia kuchemshia mboga.
- Pika mboga za majani kwa muda mfupi iwezekanavyo, na isizidi robo saa kutegemeana na aina ya mboga mboga.
- Kula au tumia mboga mara baada ya kupika. Hivyo unapaswa kupika mboga yako muda mfupi kabla ya kula.
- Mboga za majani zisiachwe kwenye hali ya uvuguvugu kwa muda mrefu kwani virutubishi vingi hupotea zaidi katika hali hiyo.

Ahsanteni sana na maandalizi mema ya mapishi.
 

Monday, December 9, 2013

Superfood that helps detoxify your body.

  Have you noticed that practically everyday a new story comes out in the media about the toxic side effects of living in a modern world? Chemical and heavy metal dangers seem to be lurking everywhere you turn in the 21 century. Pesticides coat much of our fresh food supply, chemical by-products from manufacturing are routinely dumped into our air and water, and mercury amalgam fillings in your teeth may be releasing mercury into your body with every bite of food you take.

  The seafood in our oceans are laden with heavy metals and mercury and pass these poisons up the food chain until potentially massive doses of both wind up on your dinner plate disguised as a health meal. Underground water supplies have been tainted by chemical and pesticide run off from from farms and factories.

  It doesn't take much imagination to see that you body too is under attack from environmental pollution every single day. You can seek to protect yourself and combat these hazard by eating foods that are free of pesticides and chemicals, but you simply cannot entirelly remove all sources of toxins from your environment. The damage to our world is just a wide-spread and pervasive. You have to take it upon yourself to take measures to protect yourself and your family from these toxic world, and one of the best natural sources for removing these toxic materials out of your body is an algae called "Chlorella".

  Chlorella is actually one of the most widely used supplements in Japan, where over 10 million people use it regularly. One of the reasons the Japanese value chlorella so highly is its natural detoxification abilities  Chlorella is a "green food", a single celled, micro-algae that is about two to ten microns in size.It's very small. It is this small size combined with its unique properties that make it such a useful detoxification tool. Its molecular structure, allows it to bond to metals, chemicals an pesticides.

  When chlorella is taken into your body, its natural action will bind it to lingering heavy metals, chemicals and pesticides found in your digestive tract which is your body's pathway to your bloodstream where these harmful toxins are delivered and deposited into your body's cells.

  So chlorella first and most will help your body eliminate unwanted metals and toxins. But it does more than that.

  Chlorella is uniquelly designed to not bind to the minerals your body naturally needs to function optimally. It does not bind to beneficial minerals like calcium, magnesium, or zinc. It is almost as if chlorella knows which metals belong into your body and which chemicals need to be removed. Supplementing with chlorella is like unleashing a tiny army inside your body to fight a battle of removing toxins from your tissues and ushering them back outside your body where they belong.

                                        The history of chlorella

   Chlorella is one of the most widely studied food supplements in the world. Aside from being the subject of medical research in the USA, Russia, Germany, Japan, France, England and Israel, chlorella has been extensively studied as afood source since it is made up of whopping 50 percent protein and is considered a complete amino acid-based food (complete protein).

  Even NASA has studied using chlorella as one of the first whole foods in space on the international space station.

  Studies in Japan, have shown chlorella may help reduce body fat percentage and may be useful in fighting obesity and weight related diabetes. Chlorella's cleansing action on your bowel and other elimination channels, as well as its protection of your liver, also helps promote clean blood. And clean blood helps assure that metabolic waste gets efficiently carried away from your tissues.

  Chlorella is such a powerful detoxifier because it is reach in chlorophyll which is known to;
- Aid you in processing more oxygen,
- Cleanse key elimination systems like your bowel, liver and blood.
- Help purify your blood and clean away toxins.
- Aid you in promoting optimal blood pressure.
- Support elimination of molds in your body.
- Help neutralize bad air you might breathe in.
- Promote growth and repair of your tissues.

  Chlorella is actually very useful even beyond detoxification, and its range of health benefits includes:
- Boosting your immune system.
- Improving your digestion especially if constipation is a problem.
- Providing B vitamins from an animal source.
- Enhancing your ability to focus and concentrate.
- Increasing your energy levels.
- Balancing your body's pH.
- Normalize your blood sugar and blood pressure.
- Reducing your cancer risk.
- Freshening your breath.

  Sometimes living in the modern world can feel like you are at war with the environment around you, and sources of pollution are often silent and unavoidable. Maintaining optimum wellness includes creating defensive mechanisms to fight back against these pervasive and unavoidable environmental assaults on your good health.

  By implementing a detoxification program of your body, you can help your body naturally remove the unwanted and harmful heavy metals, chemicals and pesticides you may unknowingly taken into your body. And lessening your toxic burden has been shown to improve many common health ailments, from lack of energy and insomnia, to sluggish digestion, lack of immune response and mental fatigue.

  In fact, almost everything inside your body, including all of your organs, function better with reduced loads of systemic toxins. And by removing the toxins now and not letting them accumulate to dangerous levels, you may be helping your body ward of such killers as cancer, diabetes and hypertension, along with all of the now too common Neurological disorders that may not manifest for decades to come.

 As every body know that, health is everything, you can not do anything if your health is in trouble. You can not go to farm! You can produce nothing.

Friday, December 6, 2013

KILIMO BORA CHA ALIZETI

Alizeti ni kati ya mazao yanayotoa mbegu za mafuta. Hutoa mafuta kati ya asilimia 45-55 na mashudu yake ni chalula cha mifugo. Alizeti huvumilia ukame na hulimwa kwa ajili ya biashara na matumizi ya nyumbani. Wakulima huvuna kiasi kidogo, kati ya gunia 3-5 kwa ekari. Hivyo kwa mavuno mengi na bora, mkulima anashauriwa kuzingatia mambo yafuatayo:-

1. KUANDAA SHAMBA.

Unashauriwa kutayarisha shamba lako mapema kwa kukatua ardhi na kulainisha vizuri. Samadi yaweza kuchanganywa vizuri na udongo wakati wa kuandaa shamba.

2. WAKATI WA KUPANDA.

Maeneo yenye mvua nyingi alizeti huanza kupandwa mwishoni mwa mwezi Januari mpaka katikati ya mwezi Februari. Maeneo yenye mvua kidogo alizeti hupandwa mwezi Desemba hadi Januari.

3. KIASI CHA MBEGU NA UPANDAJI.

Kiasi cha kilo 3-4 za mbegu zinatosha kupanda eneo la ekari moja. Panda mbegu 3-4 ktk kila shimo kwa nafasi ya sentimita 75 kutoka mstari hadi mstari na sentimita 30 kutoka shimo hadi shimo. Shimo la mbegu liwe na kina cha sentimita 2.5-5. Wiki mbili baada ya kuota, punguza miche katika kila shimo na kubakiza mche mmoja.

4. KIASI CHA MBOLEA.

Mbolea zinazofaa kwa kilimo cha alizeti ni zile za kupandia na kukuzia hasa kwenye maeneo yasiyo na rutuba. Wakati wa kupanda tumia nusu mfuko kwa ekari moja ya mbole ya kupandia na mfuko mmoja kwa ekari moja ya mbolea ya kukuzia kwa kuigawa mbolea hiyo mara mbili. Nusu ya kwanza iwekwe wakati wa kupanda na nusu ya pili iwekwe wiki mbili baadaye.

Note: Wakati wa kuweka mbolea angalia isigusane na mbegu au mche wa alizeti kwani huunguza.

5. PALIZI.

Alizeti hukua taratibu ktk wiki za mwanzo. Hivyo unashauriwa kupalilia mapema kupunguza hasara. Katika maeneo yaliyo na magugu machache, palizi moja tu inatosha. Vile vile maeneo yenye upepo mkali, wakati wa kupalilia inulia matuta kuzuia kuanguka.

6. FUNZA WA VITUMBA(American bollworm).

Funza huyu hutoboa mbegu changa kuanzia mara tu vitumba vya maua vikifunguka mpaka karibu na kukomaa kwa mbegu.
Tumia dawa yoyote ya kuulia wadudu.

Monday, December 2, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (4)- AINA YA MIZIZI

(i) RADISHI.

Zao la radishi hujulikana pia kama "Karoti Nyeupe", hupendwa sana na wakulima kwa sababu hustawishwa kwa urahisi na hukua haraka na kutumiwa katika muda mfupi. Asili ya zao hili ni katika nchi za Ulaya.

Ijapokuwa radishi hasa ni zao la nchi za baridi, siku hizi linastawishwa zaidi katika nchi zenye joto la kadri (Temperate zone) na katika Nyanda za juu za tropiki.

AINA: Kuna aina nyingi za radishi ambazo hutofautiana kwa umbo, ukubwa na rangi ya matunda (mizizi) yake. Aina zinazojulikana zaidi ni Chery Belle, Comet, Scarlet Globe, Sparkler, White Icicle, White Chinese, Golden Globe, French Breakfast na Sakurajima.

Mmea wa radishi ni wa msimu mmoja, lakini katika nchi za baridi mmea huu huweza kukua kwa kipindi kirefu zaidi na kutoa shina au mlingoti wenye vitawi. Chakula aina ya wanga kitengenezwacho na mmea hulundikana kwenye mzizi na kuuvimbisha. Umbo la mzizi huwa mviringo, au mviringo uliochongoka kidogo, au refu mfano wa pingili. Rangi yake ya nje ni nyekundu, au zambarau, au nyeusi, au rangi ya maziwa (cream), lakini kwa kawaida rangi ya ndani ni nyeupe. Mzizi huliwa ukiwa mbichi au baada ya kupikwa, pia majani yake huweza kupikwa na kutumiwa.

USTAWISHAJI: Zao hili huweza kuoteshwa katika aina nyingi za udongo, lakini hustawi vizuri mahali penye ardhi laini, tifutifu, au nusu kichanga mradi pawepo na rutuba ya kutosha.

Radishi hupendelea hali ya ubaridi wa kadiri, hivyo katika nchi za tropiki unashauriwa kulima zao hili katika sehemu za milimani ambako joto lake siyo kali.

KUPANDA: Radishi ni mmea wenye uwezo wa kustawi bila shida, na unaweza kuoteshwa karibu wakati wote wa mwaka. Ni vizuri mipando ya zao hili iachane kwa kipindi cha majuma mawili hivi kusudi uweze kupata mboga zake wakati wote.

Mbegu zake hutiwa kidogo kidogo katika mistari yenye kina cha sentimeta 1 hadi 2, kisha hufunikwa kidogo kwa udongo laini. Kilo 3 za mbegu hutosha robo hekta ya bustani, umbali wa mistari ni sentimeta 30 hadi 40. Baadaye miche hupunguzwa na kuacha nafasi ya 5-8 sentimeta.

FASO TANZANIA: IJUE ALIZETI INAVYOTUMIKA KAMA MALISHO YA MIFUGO.

FASO TANZANIA: IJUE ALIZETI INAVYOTUMIKA KAMA MALISHO YA MIFUGO.: Alizeti haitoi mailisho pekee, pia inatoa mafuta bora kwa afya ya binadamu na pia malighafi inayotumiwa na nyuki kutengeneza asali. ...