Wednesday, November 27, 2013

Fwd: KILIMO CHA MBOGA MBOGA (3)- AINA YA MABOGA.

---------- Forwarded message ----------
From: mmisungwi@gmail.com
Date: Wed, 27 Nov 2013 07:46:00 +0100
Subject: KILIMO CHA MBOGA MBOGA (3)- AINA YA MABOGA.
To: mmisungwi.mgonga@blogger.com

(ii) MATIKITI

Kuna aina mbili za Matikiti, Tikiti- Maji (Water Melon) na Tikiti-
Tamu (Sweet Melon). Asili yake ni Afrika na kwa sasa zao hili
linalimwa sana Afrika Magharibi na Mashariki, India, Indonesia, na
katika Visiwa vya Caribean.

Aina zilimwazo zaidi ni hizi zifuatazo;

Tomo Waston, Dixie Queen, Charleston Grey, Congo, Florida Giant. Aina
zote hizi ni Tikiti- Maji.
Ustawishaji: Zao hili hustawi toka usawa wa bahari hadi 1,000.
Huvumilia tofauti za hali ya hewa, na huhitaji unyevu wa kawaida
kutosha katika hatua za mwanzo mradi tu upungue kadri linavyokaribia
kukomaa. Unyevunyevu ukizidi sana husababisha magonjwa na kupunguza
utoaji wa maua. Pia joto kali sana hudhuru matunda.

Kupanda: Mbegu hupandwa nyakati za mvua, na matunda huvunwa nyakati
za kiangazi. Hupendelea ardhi yenye rutuba, tifutifu, na isiyotuamisha
maji. Mbolea ya takataka au samadi ndiyo ifaayo zaidi.
Mbegu hupandwa kwenye matuta au vilima vya udongo. Tia mbegu mbili
au tatu ktk shimo, baadaye ng'oa na kubakiza mche mmoja ulio na afya.
Umbali wa kupanda ni sentimeta 60 hadi 90 kati ya mimea, na sentimeta
120 hadi 180 kati ya mistari.
Ni muhimu kupalilia na kutandaza nyasi kwa kuzungushia mashina
kusudi kuzuia mizizi isidhuriwe na jua. Nyakati za ukame, umwagiliaji
ni lazima. Katika hatua fulani ya kukua, inapendekezwa kukata ncha za
mimea jambo ambalo linasababisha kutoka kwa matawi mengi pembeni
pembeni, ambayo hatimaye hubeba matunda. Matunda huwa tayari kuvunwa
baada ya majuma 12 hadi 15 tangu kupandwa.

Magonjwa: Magonjwa ya zao hili ni sawa na yale ambayo hushambulia
matango, yaani Cucumber Mosaic, Bacteria Wilt, Downy Mildew na Powdery
Mildew. Hata hivyo njia za kupigana na magonjwa hayo ni sawa na za
kwenye Matango.
Anthracnose- Ugonjwa huu hushambulia sana zao hili kuliko
unavyoshambulia mazao mengine yaliyo ktk kundi hili. Hutokea madoa
meusi kwenye matunda na sehemu zenye madoa huonekana zimebonyea.
Nyunyizia dawa ya Malathion au copper

Wadudu: Wadudu ni wale wale wa Matango, hatari zaidi ni Aphids.

Ahsanteni! sabab

Tuesday, November 26, 2013

Thanksgiving_ Dear friend, The holidays are all about excess, Overpriced gifted, Overbooked Schedules, and_ of_course too much food.

---------- Forwarded message ----------
From: "Danielle Nierenberg, Food Tank" <danielle@foodtank.org>
Date: Mon, 25 Nov 2013 16:35:00 +0000
Subject: Thanksgiving
To: Friend <mmisungwi@gmail.com>

Dear Friend,

The holidays are all about excess. Overpriced gifts, overbooked
schedules, and—of course—too much food.

Some five million tons of food—enough to fill the John Hancock
Building more than 14 times—will be wasted between Thanksgiving and
the end of 2013. Worldwide, some 1.3 billion tons of food is wasted
annually, according to the U.N. Food and Agriculture Organization.

In the United States, roughly one-third of food is thrown away as a
result of over-buying and misinterpretation of expiration and sell-by
dates. In the developing world, an equal amount of food is lost
because of poor infrastructure, pests, and disease. As a result, all
the hard work that farmers do to fertilize and irrigate crops goes to
waste, putting them further into poverty.

And while wasting food presents a moral conundrum, it also presents
environmental and social challenges that policy-makers, business
leaders, and eaters need to be solve today, not tomorrow.

Food loss and waste is insidious. A little bit is lost in fields, a
little is lost during transport, a little is lost in storage, and a
little bit is lost in homes. The amount of food wasted in the U.S.
each year totals some US$165 billion—and more than US$40 billion of
that waste comes from households, according to the Natural Resources
Defense Council.

Recently, U.N. Secretary General Ban Ki Moon called issued the Zero
Hunger Challenge, propelling nations to increase access to food,
prevent stunting, improve environmental sustainability in the food
system, and increase productivity on farms as well as reduce all food
loss and waste to zero.

And while Moon's goal may seem ambitious, they're more needed than
ever before. According to the FAO, hunger has decreased by roughly 17
percent since the early 1990s to 842 million hungry people today. But
progress has been uneven. More than 265 million people sub-Saharan
Africa alone are hungry and at least 100 million tons of essential
foods in the region are lost because of lack of roads, proper storage
facilities, and markets.

Earlier this year, Moon called for nations to correct the inequity of
food waste in a world plagued by hunger. "By reducing food waste, we
can save money and resources, minimize environmental impacts and, most
importantly, move towards a world where everyone has enough to eat,"
he urged.

Farmers, food processors and retailers, and consumers are already
taking the initiative to alleviate food loss and waste by finding
innovative ways to reduce food loss and food waste. Some of the most
interesting solutions are from organizations such as Growing Power,
which picks up and composts some 400,000 pounds of food waste from
Midwest businesses each week. In New York, City Harvest collects food
that would have otherwise been wasted from restaurants and distributes
it to those in need. And the Food Recovery Network is mobilizing
university students around the country to distribute food from college
cafeterias and catering facilities to homeless shelters.

On the other side of the world, fishers in The Gambia are smoking
abundant fish harvests. In India, farmers are drying papayas and
mangos to help make sure that families have access to vitamin A and
extra income from the sale of dried fruit throughout the year.

And in Pakistan, the United Nations helped farmers reduce grain
storage losses by up to 70 percent by replacing jute bags and mud
silos with metal grain storage containers that prevent moisture and
vermin from eating grain.

On the policy side, the U.S. Congress, the U.S. Department of
Agriculture, and the U.S. Food and Drug Administration need to work
together to ensure sell-by, expiration dates, and use-by dates are
regulated and easy for consumers to understand.

And more is needed to combat food loss and waste internationally.

This week, at the Barilla Center for Food & Nutrition 5th Annual
Forum, the Milan Protocol will be released, calling on international
leaders and food system stakeholders to improve agricultural
sustainability, control food price instability, encourage healthy food
choices, improve land rights—and combat food waste.

In 2014, the world leaders, businesses, civil society, and eaters
should resolve to make waste in the food system part of our past, not
our future.

What do you think? Email me at anytime at danielle@foodtank.org!

Onward!

Danielle Nierenberg
(http://www.DanielleNierenberg.com?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037)
Co-Founder, Food Tank
(http://www.FoodTank.org?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037)
foodtank.org
Email: danielle@foodtank.org
Phone: 202-590-1037
JOIN Food Tank:
https://foodtank.org/sustainer?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037

Get Rid of the 'Food Desert' Label LINK:
http://foodtank.org/news/2013/11/get-rid-of-the-food-desert-label?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
The food desert diagnosis too easily turns into a club used to beat
families most in need. Being labeled a food desert makes a
neighborhood undesirable, rather than a target of opportunity.

This land is our land: The struggle for land rights in Papua New Guinea
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/this-land-is-our-land-the-struggle-for-land-rights-in-papua-new-guinea?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
In Papua New Guinea, in a matter of a few years, more than 5.5 million
hectares, or 12 percent of the country, were acquired by foreign firms
through a scheme called Special Agriculture and Business Leases
(SABLs). These land deals constitute one of the swiftest and largest
land grabs in recent history.

Veteran-Veterinarian Combines Skills as Food Safety Consultant for
Farmer Veteran Coalition
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/veteran-veterinarian-combines-skills-food-safety-consultant-farmer-veteran?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
Michele Pfannenstiel uses her unique background in the army and
veterinary medicine to fill a niche as food safety consultant for
Farmer Veteran Coalition (FVC) and mobilizes other vets to use safe
farming practices.

Papaya for Haiya: Philippine Farmers Post-Taiphoon
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/papaya-for-haiya-philippine-farmers-post-taiphoon?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
Local family farm set up a pickling day - Operation: Papaya for Haiyan
- to produce jars of pickled papaya, or "achara" to be sold with all
proceeds providing medical supplies for victims of Haiyan!

Niman is a Pig's Best Friend
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/niman-is-a-pigs-best-friend?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
John and Beverly Gilbert, third-generation pig farmers, are part of
the Niman Ranch Pork Company, a nationally known marketing cooperative
that buys well-raised pork, poultry, lamb, and beef from hundreds of
small farmers across the country who meet their strict animal welfare
standards.

Why Is Obesity Soaring?
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/why-is-obesity-soaring-the-answer-is-more-complex-than-human-behavior?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
A recently published article in the New York Times suggests we should
invest as many research dollars in understanding the biology of
obesity, as we do the behavior of obesity. The results could change
the way we think about solutions and policies to prevent obesity.

Farm to School: Putting Some Crunch in Your Lunch
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/farm-to-school-putting-some-crunch-in-your-lunch?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
From farm gate to lunch plate, farm to school lunch programs are
making an impact on health, nutrition, and education of youth. Among
them an award winning farm to salad bar, run by eight middle school
students.

Seeds Define the South's Legacy
LINK: http://foodtank.org/news/2013/11/southern-seed-legacy?utm_source=Food+Tank%3A+The+Food+Think+Tank&utm_campaign=09d9467694-Holidays&utm_medium=email&utm_term=0_c6d5c4b977-09d9467694-12619037
What defines the legacy of a place? Is it its history, its citizens,
its architecture? For the Southern Seed Legacy, it's all about what
grows in the soil.





This email was sent to mmisungwi@gmail.com
why did I get this?
(http://foodtank.us5.list-manage.com/about?u=af81786f650f3d9a402f0309e&id=c6d5c4b977&e=ca82d244e3&c=09d9467694)
unsubscribe from this list
(http://foodtank.us5.list-manage1.com/unsubscribe?u=af81786f650f3d9a402f0309e&id=c6d5c4b977&e=ca82d244e3&c=09d9467694)
update subscription preferences
(http://foodtank.us5.list-manage.com/profile?u=af81786f650f3d9a402f0309e&id=c6d5c4b977&e=ca82d244e3)
Food Tank: The Food Think Tank · 4858 N. Hermitage Ave · Suite 3A ·
Chicago, IL 60640 · USA

Monday, November 25, 2013

MKULIMA TAFADHALI USINUNUE PEMBEJEO OVYO!

Ndugu zangu wakulima, ni msimu wa kilimo sasa, mvua zimekwishaanza kunyesha maeneo mengi hapa nchini. Najua mkulima yuko bize kuhakikisha anapata pembejeo za kuweka shambani mwake.
Katika harakati hizo za kupata Mbolea na Mbegu bora, mkulima anapitia changamoto nyingi.

Katika soko la Pembejeo, mkulima anatapeliwa kwa kuuziwa mbolea na mbegu feki na wafanyabiashara wadanganyifu. Baada ya hapo mkulima anakuja kulia katika mavuno. Lakini haya yote wakubwa wenye mamlaka ya juu hawayajui? Na kama wanajua je, wameamua kwa makusudi kuwaacha waendelee na wizi huu? Kila mtu ajiulize swali hilo.

Tuache yote, hebu tuangalie sasa kumsaidia na kumshauri mkulima ili angalau aepuke kwa kiasi fulani kununua pembejeo feki na ambazo hazina kiwango.
Kwanza kabisa mkulima mwenyewe kabla hajanunua pembejeo ajiulize na kuamua, mbolea ama mbegu gani anahitaji kutumia na kulima. Katika kufanikisha hilo, mambo yafuatayo yanatakiwa mkulima kuzingatia:

1. Nunua pembejeo mahali stahiki yaani kwenye maduka maalumu ya pembejeo- Hili ni muhimu sana, wakulima wengi wanaotapeliwa ni kukosa umakini katika ununuzi wa pembejeo. Kutokana biashara huria tuliyonayo, mtu anaamua tu kuanza biashara ya pembejeo bila kufuata vigezo vinavyotakiwa. Kwa hiyo chunguza mazingira ya duka unalonunua pembejeo zako, je, yanaridhisha?

2. Unaponunua pembejeo yoyote ile, hakikisha unaomba list, hii itakusaidia endapo mambo yataharibika huko shambani. Hakikisia list hiyo inaeleza mambo muhimu kama Jina kamili la duka, mahali duka lilipo, mawasiliano na aina ya bidhaa uliyonunua.
3. Angalia muda wa mwisho kutumika (expire date) kwa pembejeo uliyonunua kabla hata hujaondoka dukani.

4. Unapotumia pembejeo yoyote ile hakikisha unabakiza walai kiasi kidogo kama ushahidi katika vipimo pale inapoonekana tofauti. Hii inamrahisishia mtaalam wa kilimo aliyekaribu kupata pa kuanzia pale panapotokea tatizo.

5. Epuka kununua pembejeo vichochoroni eti kisa zina bei rahisi.

Mambo hayo matano ni ya kuzingatia sana wakati wa ununuzi wa pembejeo. Nawatakia kilimo chema.��ba li

Wednesday, November 20, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (3)- AINA YA MABOGA.

(i) MATANGO

Asili yake ni Afrika au Asia, lakini kwa sasa hustawishwa katika sehemu nyingi za kitropiki. Matunda yake hukatwa katwa na kuliwa kama achali, au kachumbali, au huwekwa kwenye siki, au hupikwa na kuliwa.

Kuna aina nyingi, lakini hutofautiana kwa umbo na rangi. Aina zinazojulika zaidi hapa kwetu ni: Colorad, Telegraph, Palmetto, Chicago, Pickling, Straight 8 na Marketer.

Ustawishaji: Zao hili huhitaji hali ya joto na hukua kwa haraka sana. Hustawi katika aina nyingi za udongo. Hatua za kupanda mbegu ni sentimeta 60 hadi 75 kati ya mimea, na hatua hizo hizo kati ya mistari. Mimea michanga inatakiwa iwekewe kinga ili isidhuriwe na upepo.
Matango hukua na kukomaa kwa haraka zaidi katika udongo mwepesi, lakini hutoa mavuno makubwa zaidi katika ardhi nzito kiasi. Hata hivyo ardhi inayotuamisha maji haifai, na ikibidi mimea ipandwe kwenye matuta.
Zao hili hutumia chakula kingi kutoka ardhini, kwa hiyo ni muhimu kuweka samadi au mbolea ya takataka mara kwa mara. Matunda huwa tayari kuvunwa baada ya majuma sita hadi manane tangu kupandwa.

Magonjwa: (a) Bacteria Wilt- Majani yaliyoshambuliwa hunyong'onyea na kudhoofu na hatimaye hufa. Mmea ukikatwa huchuruzika ute mzito. Nyunyizia dawa ya Copper kila baada ya siku 10 na tumia aina zenye uvumilivu mkubwa kama vile Palmetto.

(b)Powdery Mildew- Ukungu wake hushambulia majani na mashina. Nyunyizia dawa ya unga ya sulphur kila baada ya siku 10.

(c)Cucumber Mosaic- Husababishwa na sumu (virus). Hali ikiwa mbaya zaidi mmea hugeuka njano, hudumaa na hushindwa kutoa matunda. Huenezwa na magugu au wadudu kama aphids na beetles. Usafi bustanini unahitajika.

Wadudu: (a)Cucumber Beetle- Huyu ni mdudu mbaya sana kwa zao hili. Hutafuna miche ya matango na maboga mara ichipuapo, pia hushambulia majani ya mimea michanga.

(b)Melon Aphid- Hufyonza utomvu wa mimea. Tumia Malathion,Nicotine. Hakisha dawa inafikia upande wa chini wa majani

(c)Pickle Worm- Buu au funza hujipenyeza ndani ya ua,kisha huhamia kwenye tunda.Tumia Rotenone au Crylite kila baada ya juma 1.��hina.

Tuesday, November 19, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA

(v) BAMIA

Asili ya mboga hii ni Afrika ya Kati na ya Mashariki, lakini kwa sasa zao hili limekwisha enea katika sehemu nyingi za kitropiki, kama Visiwa vya Caribbean, Malaysia na Philipines.

Urefu wa mmea huwa kati ya meta moja na mbili. Matunda yake hufikia urefu wa sentimeta 10 hadi 20, na huchumwa kabla hayajakomaa sana na hupikwa pamoja na nyama, samaki au mboga nyingine. Majani yake huchumwa yakiwa bado machanga na kutumiwa kama mboga nyingine za majani.

Aina za bamia zinazojulikana zaidi ni Clemson Spineless, Emerald Green, White Velvet, Perkins Mammoth na Dwarf Prolific.

Ustawishaji: Zao hili hustawi katika mete 1000 kutoka usawa wa bahari na hushindwa kuvumilia hali ya baridi kali. Hustawi katika katika aina nyingi za udongo na huhitaji mvua za wastani. Mimea yake haitumii chakula kingi kutoka ardhini. Iwapo ardhi haina rutuba ya kutosha inapendekezwa kuweka mbolea ya takataka au samadi.

Kupanda: Kwa kawaida mbega za bamia hupandwa moja kwa moja katika bustani, lakini pia kwanza zinaweza kupandwa kwenye kitalu na kuhamishwa baadaye. Mbegu zimiminwe kidogo kidogo na miche ifikiapo urefu wa sentimeta 10 hadi 15, idadi yake ipunguzwe. Umbali wa unaopendekezwa ni sentimeta 40-50 kati ya mimea na sentimeta 70-80 kati ya mistari. Kilo moja hadi moja na nusu ya mbegu hutosha robo hekta ya bustani (zaidi ya nusu eka hivi).

Mbegu za bamia huota kwa shida, mara nyingi huchukua siku nane hadi 12 kutokeza. Ili kurahisisha uotaji, inapendekezwa kwanza kuweka mbegu katika chombo chenye maji ya vuguvugu kwa muda wa saa 24.
Iwapo unyevu wa ardhi hautoshi, inapendekezwa kutumia mojawapo ya njia za kumwagilia maji bustanini. Mimea ifikiapo urefu wa nusu meta hivi wakulima wengine huondo ncha zake kwa kuamini kwamba wingi na ubora wa matunda huongezeka. Bamia huwa tayari kuchumwa baada ya miezi 2 tangu kupandwa na huendelea kwa muda mrefu.

Magonjwa: Mosaic Virus- Huu ni ugonjwa mbaya sana, majani huwa na madoamadoa na huumbuka. Haki hii hupunguza mazao. Nyunyizia dawa za sumu kuua wadudu.

Monday, November 18, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA

(iv) NYANYA MSHUMAA.

Zao hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo". Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya.

Mmea hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo.
Rangi ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga zingine. Pia hupikwa pamoja na ndizi.

Kupanda: Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi 15 hupandikizwa bustanini, kwa umbali wa sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya "Ngogwe" hutunzwa kama bilinganya, huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu kidogo.

Maadui: Nyanya Mshumaa ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na baadhi ya Magonjwa yasababishwayo na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao hushambulia zao hili, madhara ya si makubwa sana kiasi cha kutisha au kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.

Kuvuna: Mboga huvunwa wakati zikiwa bado mbichi. Ili ziweze kukaa kwa muda mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi masoko ya mbali bila kuharibika.

Mkulima ongeza uzalishaji katika mazao ya mboga mboga ukuze uchumi wako.

Thursday, November 14, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA

(iii) PILIPILI
Pilipili ni kiungo kikali, hutumiwa kwa kukoleza mchuzi na vyakula mbali mbali. Pilipili zinaweza kupikwa zikiwa nzima au kukatwakatwa na kutumiwa katika kachumbari; au kuwekwa kwenye siki na achali, au kusagwa na kutumia unga wake.
Hili ni zao la nchi za kitropiki, na hutumiwa sana na wakazi wa Bara Hindi, Mashariki ya Mbali. Amerika ya Kusini na Afrika ya Tropiki. Pilipili huwekwa katika makundi makubwa mawili, yaani:
1. Pilipili Hoho (Hot Pepper)- Hizi ni ndogo ndogo, ndefu, nyembamba, na kali sana. Aina zinazojulikana zaidi ni Green Chilli, Cherry Pepper, Long Cayenne na Tabasco.

2. Pilipili Manga (Sweet Pepper)- Hizi zina umbo kubwa, nyama nying, mviringo na ndefu kidogo, siyo kali. Aina zinazojulikana zaidi ni Sweet, Neapolitan, Keystone, Giant, Ynlo Wonder na california wonder.

Kupanda: Mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma manane hadi kumi. Kisha miche hupandikizwa bustani kwa umbali wa sentimeta 45 kwa 90.

Kuvuna: Umri wa kuvuna zao hili hutegemea aina ya pilipili na matumizi yake. Aina ambayo ni kubwa na tamu kwa kawaida huvunwa kabla haijapevuka na kugeuka rangi yake. Pilipili katika hali hii hutumiwa zaidi kwenye michuzi, kachumbali na kutiwa kwenye makopo.
Pilipili kali, ambayo mara nyingi ni ndogo ndogo, kwa kawaida huvunwa baada ya kupevuka na kuwa nyekundu. Halafu hutumiwa katika mapishi na vyakula mbali mbali, lakini sehemu kubwa zaidi hukaushwa na kusagwa ili kupata unga wake.

Magonjwa: Damping- off, Bacteria Spot, Fusarium wilt na Antracnose, ni miongoni mwa magonjwa yashambuliayo zao hili. Tuseme magonjwa ya pilipili ni sawa na ya Nyanya. Hivyo njia za kupigana nayo ni sawa.

Wadudu: Wadudu ambao hushambulia zao hi wengi, lakini walio wabaya zaidi ni Aphids, Cut worm, Flea beetle, Pepper weevil na Pepper Maggot.

Kinga: Parathion 1% au Chlrdane 5%. Dawa itumiwe mara wadudu watokeapo na kurudiwa kila baada ya siku 7.

Ahsanteni!

Wednesday, November 13, 2013

BIG RESULTS NOW! Malaysia na Tanzania.

  Kwanza kabisa kila mtanzania kwa sasa anajua na kulisikia sana neno hili la "Big Results Now" Matokeo makubwa sasa. Mfumo huu serikali imeamua kuuchukua kutoka nchi ya Malaysia ambako ilionekana kuwanufaisha na kukuza uchumi wao kwa haraka. Hebu tuziangalie hizi nchi mbili sasa.

Wakati Tanganyika inapata uhuru mwaka 1961, nchi ya Malaya ilikuwa tayari ina uhuru mwaka 1957. Malaya ilijiunga na Singapore, Sabah na Sarawak mwaka 1963 na kuunda Malaysia. Tanganyika yenyewe ilijiunga Zanzibar 1964 kuunda Tanzania. Hata hivyo Singapore ilifukuzwa katika muungano huo mwaka 1965. Nchi zote hizi mbili zilitawaliwa na Mwingereza.

  Wakati Tanzania inaundwa mwaka 1964, pato la wastani la mtu mmoja lilikuwa ni USdolar 63, wakati Malaysia ilikuwa USdolar 113. Kimsingi nchi hizi zilikuwa sawa kimaendeleo ingawa Tanzania ni kubwa mara tatu ya Malaysia.

  Hivi sasa Malaysia kipato cha wastani cha mwananchi ni USdolar10,000 na Tanzania ni USdolar 600. Kwa Tanzania pato limeongezeka mara kumi na Malaysia limeongezeka mara elfu moja.
Nini tofauti ya mikakati ya nchi hizi mbili?

  Leo hebu tuangalie eneo moja tu la Kilimo, na namna Kilimo kilivyoweza kuivusha nchi ya Malaysia na Kilimo hicho hicho bado hakijaweza kuivusha Tanzania.
Malaysia iliunda Shirika la Umma, Federal Land Development Authority, (FELDA) likiwa na wajibu mmoja mkubwa wa kuhakikisha wananchi masikini wanapata ardhi, wanlima kisasa na kuongeza uzalishaji, kisha kufuta umasikini.

  Kila mwananchi masikini aligawiwa hekta 4.1, ardhi ikasafishwa na kuwekewa miundombinu ya muhimu, ikapandwa michikichi na mwananchi akapata huduma za ugani ili kukuza michikichi hiyo. Shughuli zote hizi zilifanywa kwa gharama za Serikali na wananchi wote waliowezeshwa wakapewa kama mkopo ambao walikuwa wanaulipa kidogo kidogo kila wanapovuna na kuuza Mawese kwa Shirika hili la Serikali. Hivi sasa Shirika hili ni kubwa sana, lina thamani USdolar bilioni 3.5 na kupitia ushirika wao wananchi hawa waliopewa ardhi ya kulima michikichi sasa wanamiliki 20% ya Shirika hili.
Malaysia iliweza kuondoa umasikini kutoka 57% ya wananchi wanaoishi kwenye dimbwi la umasikini mwaka 1965 mpaka chini ya 3% mwaka 2012.

  FELDA sasa ni Shirika la Kimataifa maana linaanza kuwekeza duniani kote. FELDA ilipouza hisa zake kwenye masoko ya mitaji, IPO yake ilikuwa ni ya tatu kwa ukubwa baada ya Facebook na Japanese Airlines. Shirika la Umma linalomilikiwa na Serikali, Wakulima na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (EPF) na linaloendeshwa kwa misingkini ya utawala wa Makampuni limeweza kufuta umasikini kwa zao moja tu la Michikichi. Malaysia leo inaongoza kwa kuuza Mawese duniani. Michikichi hiyo ilitoka Tanzania na kupelekwa  Malaya na waingereza miaka ya hamsini.

  Tanzania nasi tulikuwa na Shirika la Umma kwa ajili ya Kilimo. Tuchukulie Shirika la NARCO kama FELDA, NARCO walichukua ardhi kubwa maeneo kadhaa nchini. Tofauti na FELDA wao walilima wenyewe mashamba haya na kuweka miundombinu ya Kilimo.
Tuchukulie mfano wa mashamba ya mpunga kule Kapunga, wilaya ya Mbalali Mkoa wa Mbeya. Mwaka 1985 NARCO walikwenda kijijini Kapunga kuwaomba wananchi wawape ardhi ya kulima mpunga. Wananchi wakawapa hekta 3000 hivi. NARCO wakapata msaada kutoka katika Serikali ya Japani na uwekezaji mkubwa ukafanyika ikiwemo kuweka kinu cha kukoboa mpunga cha kisasa kabisa.

  Hata hivyo NARCO ilijiendesha kwa hasara na ilipofika katikati ya miaka ya 90 ikaamriwa kubinafsishwa. NARCO ikauza mashamba yale kwa mpango wa ubinafsishwaji kwa Makampuni binafsi. Katika uuzaji huo NARCO waliuza hekta 3500 badala ya 3000 walizopewa na wananchi, kwa maana hiyo kijiji cha Kapunga nacho kiliuzwa.

  Mifano hii miwili inaonyesha tofuti kubwa za kifikra kimaendeleo kati ya nchi zetu hizi mbili. Moja iliwezesha wananchi kumiliki ardhi na imefanikiwa. Na nyingine iliamua kufanya kupitia Shirika la Umma na baada ya kushindwa, badala ya kurejesha ardhi kwa wananchi na kuwawezesha kulima, ardhi ile ikauzwa kwa kampuni ya mtu mmoja. Mfano wa Kapunga uko pia huko wilayani Hanang kwenye mashamba ya Ngano ya Basotu n.k.

  Hata kwenye mpango wa SACGOTT bado fikra ni za wakulima wakubwa wenye mashamba makubwa badala ya kuwawezesha wananchi kumiliki ardhi na kulima kwa mfumo ambao huduma zitatolewa kwa pamoja. Ujamaa wa Malaysia ulikuwa ni wa kumilikisha wananchi wao ardhi na kuwawezesha kuzalisha.
UJamaa wetu ulikuwa ni wa kumiliki kwa pamoja na hivyo kukosa uwajibikaji. Badala ya kuboresha na kuwawezesha wakulima wadogo wadogo, wakubwa wanaona ni bora kwwenda kwa wakulima wakubwa na kugawa ardhi hovyo bila mpango.

  Kwa mantiki hiyo kweli "Big Results Now" itafanikiwa? Kosa ninaloliona mimi hapa, Serikali imechukua mfumo huu kutoka Malaysia ambao wao wliweka mpango dhabiti na kuuandikikia kitabu wakikiita  "Big Fast Results" huku wakiweka miundombinu ya kutosha kuuwezesha mpango kutimia. Wakati sisi tunaoiga mfumo huu tunataka" matokeo makubwa sasa" lakini hatuna mipango ya kupata hayo matokeo sasa.

Je, hatuwezi kujifunza kwa wenzetu kweli?  Lini tutaacha Umazwazwa?

  
 

Monday, November 11, 2013

UGONJWA WA MATUPA KWENYE MAHINDI (SMUT).



    Ugonjwa huu hushambulia sehemu za uzazi za mahindi. Mashambulizi hufanywa na aina mbili za vimelea jamii ya uyoga (ukungu) vijulikanavyo kwa majina ya kitaalamu kama Sphacelotheca reliana  na Ustilago maydis. Vimelea hivyo husababisha magonjwa ya aina mbili ambayo dalili zake zinafanana.

    Mimea iliyoshambuliwa na ugonjwa huu ama haizai kabisa ama inazaa kiasi kidogo ukilinganisha na jinsi ambavyo ingeweza kuzaa kama isingekuwa imeshambuliwa. Kwa hiyo mashambulizi ya magonjwa haya husababisha hasara ya mavuno. Inakadiriwa kwamba hasara ya mavuno inawezakuwa kidogo tu ama asilimia kumi (10%) au hata zaidi ya kiwango hicho, lakini kupoteza ni kpoteza hata kama ni kiwango kidogo.

    Ugonjwa wa "matupa" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kama Ustilago maydis hufahamika kama "Common Smut" kwa kiingereza. Dalili zake huwa kuota kwa uvimbe katika sehemu za mmea zinazokua kama vile punje za mahindi, mbelewele na hata kwenye majani. Uvimbe huo ukikauka na kupasuka hutoa vumbi jeusi kama masizi ambayo ndiyo viini vya/mbegu ya huo ugonjwa. Dalili ya msingi ya ugonjwa huu kwenye mhindi ni kwamba inawezekana kuwa na baadhi ya punje zilizoshambuliwa na zingine ambazo hazina dalili katika gunzi moja.

   Ugonjwa wa "smut" unaosababishwa na kimelea kijulikanacho kwa jina Sphacelotheca reliana hufahamika kama "Head smut" kwa kiingereza. Kama ilivyo kwa ugonjwa wa "smut" ya kawaida, dalili za ugonjwa huu hujitokeza mara nyingi katika hindi lenyewe  na mbelewele na mara chache katika shina la mhindi. Tofauti na ugonjwa wa "smut" ya kawida, katika ugonjwa huu badala ya mhindi kuathiriwa baadhi ya punje, hindi zima hujaa vumbi jeusi ndani ambapo kwa nje ni kama mfuko mweupe ambao kabla ya kukauka hufana na uyoga. Vumbi hilo jeusi ndilo viini vya kimelea. Vivyo hivyo kwenye mbelewele. Wakati mwingine mmea ulioshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa na hushindwa kuzaa. Dalili nyingine ya ugonjwa huu ni mhindi kuotesha vijani vidogo badala ya mbelewele.

                                                Dalili za ugonjwa wa "Head smut"

    UDHIBITI WA MAGONJWA YA"SMUT"

1. Tumia mbegu bora ingawa mpaka sasa haipo mbegu maalumu yenye kustahimili ugonjwa huu. Kwa kutumia mbegu bora, mkulima utajihakikishia  mavuno bora.

2.  Daima hakikisha unalima kilimo cha kisasa kikijumuisha urutubishaji wa udongo. Epuka kuijeruhi mimea uwapo shambani. Mimea iliyo na majeraha hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa huu. Pia dhibiti wadudu waharibifu ambao pamoja na madhara  mengine wanayosababisha pia huijeruhi mimea na kwa hivyo kurahisisha maambukizo ya ugonjwa huu wa "smut".

3.  Kila inapowezekana tumia kilimo cha kubadilisha mazao. Katika kubadilisha mazao ni vema kutumia mzunguko wa mazao yasiyoshambuliwa na ugonjwa wa "smut" kama vile ngano, shayiri, njegere, viazi na maharagwe.

4.  Unapolima hakikisha masalia mabua yamefukiwa chini sana.

Nawatakia wakulima wote maandalizi mema ya msimu wa kilimo.

Sunday, November 10, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA.

(ii) BILINGANYA

Zao hili hustawi zaidi katika nchi za joto, hasa kusini mwa Asia, Mashariki ya Mbali na Afrika.

(a) AINA ZAKE
Kama ilivyo kwa mazao mengine, ziko aina nyingi za bilinganya ambazo hutambuliwa kwa tofauti za maumbile, sura na rangi na hujulikana kwa majina mbali mbali. Aina zinazojulikana zaidi ni: Black Beauty na Early Purple, ambazo ni za mviringo na: Florida High na Sadohara Purple, ambazo ni ndefu nyembamba.

(b) HALI YA HEWA
Bilinganya ni mmea uchukuao muda mrefu kukua, na hauna nguvu nyingi. Huhitaji hali ya joto katika muda wote wa kustawi. Baridi kali huweza kudumaza na pengine kuua mmea.

(c) HALI YA UDONGO
Zao hili huhitaji udongo laini na unyevu wa wastani. Ardhi iwe na rutuba ya kutosha, na kila inapowezekana ni bora kutumia samadi au mbolea ya takataka. Utayarishaji wa ardhi na bustani ni kama vile kwa mazao mengine ya mboga.

(d) KUPANDA NA KUTUNZA.
Kwa kawaida mbegu hupandwa kwenye kitalu ambamo hukaa kwa muda wa majuma 8 hadi 10. Kisha miche hung'olewa na kupandikizwa kwenye bustani.
Umbali wa kupanda miche ni sentimeta 60 hadi 90 kati ya mmea, na sentimeta 90 hadi 120 kati ya mistari. Unatakiwa kutifuatifua udongo wa juu mara kwa mara na kila inapolazimika uongezaji wa maji licha ya kutegemea mvua.

(e) MAGONJWA
Kuna magonjwa makubwa mawili ya zao hili, nayo ni:
Fruit Rot: Ugonjwa huu husababishwa na vimelea na hushambulia sehemu zote za mmea isipokuwa mizizi. Majani huwa na madoa ya hudhurungi. Mashina (hasa ya miche michanga) hushambuliwa, na mara nyingi huoza. Matunda nayo hupata madoa hatimaye sehemu zenye athari hiyo hulainika na kuoza. Hakuna dawa maalum ya kuzuia, inashauriwa kubadilisha mpando na kupanda aina zenye uvumilivu.
Wilt: Dalili za ugonjwa huu ni kwamba rangi ya majani hugeuka njano, halafu hupukutika kidogo kidogo. Mimea hudumaa na kufa kabla ya kukomaa

(f)WADUDU
1. Beetles na Aphids- huathiri mimea michanga
2. Lacebug- hufyonza utomvu wa mmea
Kwa wadudu hawa wote, tumia sumu yoyote kama Malathion 5%, Thiodane n.k

Bilinganya husaidia kulainisha usingizi.

Saturday, November 9, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA.

(i) NYANYA

(d) MAGONJWA YA NYANYA.
Kuna magonjwa mengi ambayo hushambulia sehemu zote za mmea wa nyanya. Baadhi ya magonjwa husababishwa na ukungu (fungus), vimelea (bacteria) na sumu (virus). Vile vile kuna magonjwa ya kunyauka au kuoza ambayo husababishwa na hali mbaya ya hewa . Magonjwa yaliyo mabaya sana ni:

1. Fusarium Wilt: Ugonjwa huu ni mbaya sana na husababisha mmea kudhoofu na majani kujikunjakunja. Rangi ya majani hugeuka njano, hatimaye kufa kuanzia chini kuelekea juu. Mimea iliyoambukizwa lazima ing'olewe na kuchomwa moto. Mpaka sasa haijapatikana dawa maalumu ya kuzuia ugonjwa huu. Kwa kuwa ukungu usababishao ugonjwa huu huishi ardhini, ni lazima kutibu udongo au kupanda aina zinazovumilia.

2. Bacteria Wilt:
Hustawi zaidi ktk hali ya joto. Mimea hudhoofu ghafla. Shina likikatwa hutoa ute mweupe na mzito. Vimelea visababishavyo ugonjwa huu huishi ardhini. Huzuiwa kwa kunyunyiziwa copper kila baada ya siku kumi. Mimea yote iliyoshambuliwa sharti ing'olewe na kuchomwa moto. Sehemu hiyo isipandwe nyanya, bilingani, pilipili au viazi mviringo kwa muda wa miaka minne ifuatayo.

3. Early Blight:
Huu ni ugonjwa wa kawaida lakini waweza kuleta hasara kubwa. Zaidi hushambuliwa miche na mimea michanga ambayo mashina yake huoza kwa chini. Majani hupata madoa ambayo huendelea kupanuka, na hatimaye baadhi ya majani hupukutika. Ni muhimu kutibu mbegu kabla ya kuzipanda. Dawa zenye asili ya copper au sulphur huweza kuzuia ugonjwa huu. Usipande mimea asili ya nyanya ktk eneo hilo.

4. Blossom - End Rot:
Huu ni ugonjwa wa matunda, husababishwa na hali mbaya ya hewa, hasa ukame. Huozesha robo hadi nusu ya tunda. Hutokea pia nyakati za mvua nyingi zifanyazo udongo kuwa tope. Kupunguza ugonjwa huu ni kuhakikisha kuwa ardhi ina unyevu wa kutosha wakati wa kupanda.

Pia kuna magonjwa mengi kama Leaf spot, Tomato Mosaic na Anthracnose.
Magonjwa yote yanaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za sumu kama Diathane M45, Thiodan n.k

(e) WADUDU.
Kuna aina nyingi, lakini wanazuiwa kwa kupiga madawa kama Thiodan, Malathion n.k ��mu ku

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (2)- MATUNDA.

(i) NYANYA.
Baada ya kutoa maelezo ya jumla kuhusu kilimo cha mboga katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hii, nilisema kwamba mboga huwekwa katika makundi matano, yaani Matunda, Majani, Mizizi, Mashina na Maua. Mboga hizi nitazieleza kwa kufuata makundi zilimowekwa.
Leo tutaanza na Nyanya katika kundi la Matunda.

Nyanya ni mboga inayolimwa na kuliwa kwa wingi hapa nchini kwetu Tanzania na duniani kote kuliko aina nyingine yoyote ya mboga. Nyanya huweza kuliwa zikiwa mbichi, au kupikwa na kuwa mchuzi au supu. Vile vile ni kiungo kikubwa ktk mapishi mbali mbali ya vitoweo na michuzi. Pia Nyanya hutumika ktk kutengeneza masala, siki, kachumbari na kadhalika. Mikoa inayolima kwa wingi Nyanya ni Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa na Mbeya, na kiasi flani kanda ya ziwa hasa Mwanza, Musoma na Bukoba.

(a) AINA ZA NYANYA.
Ziko aina nyingi za Nyanya. Hata hivyo, kiasi cha aina 10 hadi 15 ndizo zilimwazo kwa wingi zaidi.
Katika kuchagua aina za kupanda ni muhimu kuzingatia yafuatayo:
(i) Sababu ya kustawisha nyanya; kula au kuuza.
(ii) Muda uliopo wa kuzistawisha.
(iii) Wingi wa mavuno.
(iv) Ustahimilivu wa magonjwa na kutopasukapasuka.
(v) Umbo la sura yake.
Miongoni mwa aina za Nyanya ambazo hustawishwa sana na wakulima wetu ni Money Maker, Marglobe, Rutgers, Amateur, Potentate, Oxheart, Earliana, Urbana na Best of All.
(b) HALI YA HEWA.
Nyanya hupendelea hali ya joto, lakini kukiwa na unyevu wa kutosha ardhini. Mvua nyingi husababisha mimea kushambuliwa na magonjwa. Upepo mkali husababisha kupukutika kwa maua na hatimaye kupungua kwa mavuno.
(c) HALI YA UDONGO.
Nyanya huweza kustawi ktk aina nyingi za udongo. Hata hivyo udongo mwepesi au ulio nusu kichanga na nusu mfinyanzi ndio ufaao zaidi. Zao hili halipendelei ardhi yenye maji maji, lakini ni muhimu kuwepo na unyevu wa kutosha ktk muda wote wa kukua.
Makala hii itaendelea katika kipindi kinachofuata ktk sehemu hii ya pili na nitaeleza kwa undani magonjwa ya nyanya, wadudu na tiba yake.
Stay tuned Mkulima uelimike.

Friday, November 8, 2013

KILIMO CHA MBOGA MBOGA (1).

Mboga ni moja ya vyakula vilivyo muhimu sana kwa uhai wa afya ya binadamu. Mara nyingi mboga hutumiwa kama kitoweo, aina nyingi za mboga huwa na wingi wa Vitamini C, Carotene, ambayo hatimaye hubadilishwa kuwa Vitamin A, Calcium, chuma pamoja na madini mengine.
Mboga ni jina litumikalo kwa aina nyingi za mimea itumiwayo na binadamu kama chakula au kutowelea chakula kingine. Mboga hizo huwekwa katika makundi matano, yaani:

1. Matunda (nyanya, bilinganya, bamia, matango, pilipili na maharage).
2. Majani (kabeji, letusi, seleri, mchicha na mlenda)
3. Mizizi (karoti, radishi na tanipu)
4. Mashina (vitunguu maji, vitunguu saumu na iliki)
5. Maua (koliflawa na brokoli)

Pengine utajiuliza kwa nini usumbuke kulima mboga zako mwenyewe? Zifuatazo ndizo sababu kubwa za kufanya hivyo:
1. Kupata na kutumia mboga zikiwa katika hali ya upya(hazijaanza kuharibika)
2. Ni rahisi, yaani gharama ya kuzistawisha ni ndogo ukilinganisha na bei ya kuzinunua. Isitoshe aina nyingine za mboga huwa na faida mbili, kwa mfano: kunde, maharage na maboga, hutumiwa tunda na majani yake.
3. Raha ya kufanikiwa; tabia ya binadamu ni kufurahia matunda mazuri ya jasho lake, kwani binadamu hupata uradhi kwa kufanya kazi yake mwenyewe na kufanikiwa.
Baada ya mkulima kuamua kustawisha mboga katika bustani yake mwenyewe, yabidi pia ajiweke katika hali ya kupata mavuno mengi iwezekanavyo. Jambo hili linaweza kutimizwa kwa kuzingatia yafuatayo:
a) Kujua aina ya mboga ziwezazo kustawi vizuri kwa kulingana na mazingira yaliyopo, hasa hali ya hewa na udongo.
b) Kujua muda zichukuao hadi kukomaa kusudi mpango wa kufuatisha nyingine ufanywe mapema.
c) Kufahamu aina na kiasi cha mbolea zinazohitajika kutumiwa, na kufanya mipango ya kuipata wakati inapotakiwa.
d) Kufahamu magonjwa na wadudu washambuliao mboga katika eneo lake(mkulima) analo ishi, na kujua jinsi ya kupambana nao.

Ulimaji wa mboga unaweza ukawekwa katika makundi mawili; bustani ndogo ndogo karibu na makazi yetu, na mashamba makubwa kwa ajili ya biashara.
Leo nakomea hapa.

MKULIMA KUWA MAKINI NA MBOLEA YA MAJI-(SUPER GRO).

Ndugu zangu wakulima, nafahamu kwamba mnajiandaa na msimu wa kilimo sasa. Na najua pia changamoto mnazokumbana nazo kwenye maandalizi ya kuhudumia mashamba yetu, na kati ya mahitaji makubwa ni mbolea.
Wakati kama huu ndio wa kuwa makini sana hasa katika suala la uandaaji wa mbolea maana wapo watu ambao hutumia fursa hii kupita kwa wakulima na kuwahadaa, lengo lao likiwa ni kujipatia kipato.
Kuna watu wanapita pita sana wakitangaza na kunadi mbolea moja hivi ya maji, "Super Gro" watu hawa wanatoka katika shirika la GNLD, wanapita sana huku wilayani mbozi hasa katika kata za Isansa, Igamba na Msiya.
Mimi binafsi nimekutana watu hao, nilipewa taarifa na mtendaji wangu kwamba kuna wageni wanakuja na kazi yao hasa ni kukutana na kuongea na wakulima, wanatangaza na kuuza mbolea yao ijulikanayo kama super gro. Mimi kama mtaalamu wa kilimo niliwaeleza na kuwaandaa watu kwa kusaidiana na mtendaji wangu. Siku ikafika ya ujio huo. Alikuja dada mmoja na kuanza kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi na faida za mbolea hii ya maji, wakamsikiliza. Alipomaliza wakulima wakamuuliza maswali, katika maswali ndipo nilipopata mashaka na ujio huo ikabidi nifuatilie kwa undani mchakato na uhalisia wa mbolea hii.
Kwanza ki uhalisia hii siyo mbolea kwa ajili ya nafaka maana haina kirutubishi hata kimoja kinachofaa kwa Mhindi na mazao mengine ya nafaka, ni kirutubishi cha majani tu na si punje, inafaa kwenye mboga mboga.
Viambata(ingredients) yake ni kama ifuatavyo;

1. Ethoxylated- chemical hii inatumika inapunguza uwezekano wa maji kupotea, inatunza unyevunyevu (surfactants).

2. Alkylphenols- kiambata hiki kinatumika katika viwanda vya sabuni(detergents) na bidhaa za kusafishia(cleaning products).

3. Polysiloxane- inatumika kwenye viwanda vya plasitic(polymers).

Kwa maelezo yake ni kwamba unapandia mpaka kukuzia, hauhitaji kuweka mbolea nyingine, acha mkulima, hii si mbolea, itumie tu kwa kurutubisha na kustawisha majani na endelea kutumia mbolea za kawaida kama kawaida.
Huo ni ushauri wangu kwako mkulima.
Ahsante!

Thursday, November 7, 2013

Fwd: MPANGO WA MIKOPO YA PEMBEJEO.

---------- Forwarded message ----------
From: mmisungwi@gmail.com
Date: Thu, 7 Nov 2013 21:08:00 +0400
Subject: MPANGO WA MIKOPO YA PEMBEJEO.
To: misungwi.mgonga@blogger.com

Mwaka jana serikali iliamua kuleta utaratibu mpya wa upatikanaji wa
pembejeo kwa mkulima, ambao unategemewa kuanza msimu huu. Utaratibu
huu ni wa "mkopo wa pembejeo kwa mkulima" kupitia vikundi hasa AMCOS
na SACCOS. Utalenga hasa kwenye zao la mahindi ili kuzalisha chakula
cha kutosha. Pesa hiyo itajizungusha yenyewe kila mwaka.
Ni mpango mzuri sana ambao kama utasimamiwa vizuri utamkomboa
mkulima mdogo mdogo ambaye hasa ndiye mwenye kuchukua changamoto
nyingi za kilimo. Utaratibu huu uko hivi: Mkulima anatakiwa atoe 20%
ya pembejeo anazohitaji kama hisa kwenye kikundi au ushirika. Serikali
itamkopesha 80% iliyobaki. Baada ya kuvuna mkulima atatakiwa apeleke
mazao yake ghalani, masoko yatatafutwa na mkulima atalipa deni kwa
serikali kwa riba isiyozidi 5% na mkulima huyu atabaki na salio
lililobaki. Ni mpango mzuri sana. Utamnufaisha sana mkulima.
Lakini sasa changamoto zipo nyingi sana kwenye mpango huu kama vile:

1. Upatikanaji wa pembejeo kwa wakati kwa mkulima-Je, mbegu na mbolea
zitamfikia mkulima kwa wakati? au zitafika mwezi january! Hii inaihusu
serikali kuwahi kutoa 80% ili mawakala waweze kusambaza kwa wakati.

2. Urejeshaji wa mkopo- Hii inamhusu mkulima, utashi wake katika hili.
Mkulima atachukua mbegu na mbolea, atalima, Je, atapeleka ghalani? Na
pia kama hautakuwepo usimamizi dhabiti, wapo watakaochukua na
asizipeleke shambani, anauza.

3. Pembejeo kutosheleza mahitaji kwa wakati- Je, serikali itatoa kwa
wakati mmoja mahitaji ya wakulima wote? Kwa mfano katika kijiji changu
20% ni 5.4milioni, zitakuja zote kwa pamoja? Labda katika hili
ningetoa ushauri kwamba wangepiga mahesabu ya kiasi cha mbegu na
mbolea ya kupandia ndizo ziwahi mapema, kisha wale mbolea ya kukuzia
endapo pesa ya mkupuo haipo.

Hizo changamoto tatu zinatakiwa kuangaliwa sana, maana zinaweza
kukwamisha mpango mzima.
Mpaka sasa hazijaanza kusambazwa, lakini ni matumaini yangu kuwa
zitawahi mapema mwezi huu wa November.
Ahsanteni sana na karibuni kwa michango na maoni yenu katika hili.

Wednesday, November 6, 2013

UTI WA MGONGO WA TAIFA UMEKUFA

  Habari ndugu zangu watanzania, ni matumaini hamjambo nyote. Poleni na shughuli za ujenzi wa Taifa, wakulima wanahangaika kuandaa mashamba maana maeneo mengi ya nchi mvua zimeanza kunyesha sasa, poleni sana na nawaomba muongeze nguvu zenu mashambani. Ndugu zangu, leo hebu tujaribu kuangalia hili la kwamba walau kila mtanzania ama anajua, amesikia au kuambiwa kuwa Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa. Wakubwa, wenye mamlaka wamekuwa wakituimbia kila leo huo wimbo, ni wimbo mzuri sana, lakini je wanaouimba na kuutangaza unatoka mioyoni mwao na kweli uko akilini mwao hasa? Hebu kila mmoja wetu ajiulize mara mbili mbili wakati tunaenda kulijadili hili.
  Kwanza kabisa nakubaliana na hoja hiyo ya kwamba Kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu (Tanzania). Na naelewa na kuamini kwamba mlinzi hasa wa uhai wa uti wa mgongo huu si mwingine bali Mkulima, tena si mkulima tu, Mkulima mdogo mdogo wa huku vijijini. Ndugu zangu ili tuite Kilimo ni uti wa mgongo kuna vitu na mambo mengi ya kufanya kwenye hilo na si kusema tu kwa maneno.
  Mkulima anakabiliwa na changamoto nyingi sana kwenye Kilimo chake. Ili mkulima apate tija katika kilimo chake kuna vitu vinavyohitajika shambani, yaani mbolea, mbegu na madawa (Pembejeo). Pembejeo zinahitaji pesa. Mkulima anahangaika huku na kule kudunduliza kupata mbolea, changamoto nyingi anazipata wakati akihangaika kupata pembejeo ni pamoja na kupata pembejeo feki ama zimechakachuliwa au zimekwisha muda wa kutumika. Huyu mkulima anapovuna mazao yake, je soko la uhakika la mkulima huyu liko wapi? ni dhahiri shairi halipo, anahangaika tena kutafuta soko, sokoni ananyanyaswa, anapangiwa bei ya mazao yake na wafanyabiashara, hana haki tena katika mazao yake. Mfanyabiashara huyu anayempangia mkulima bei ya mazao yake, amemsaidia nini katika kuzalisha mazao yake? hakipo alichomsadia. Kwa nini basi serikali isidhibiti, kuratibu na kusimamia utaratibu wote wa masoko ili kulinda maslahi ya mkulima na mazao yake.
  Katika hilo la wajibu wa serikali, ni mipango mingi ya kumhusu mkulima anayoibuliwa, lakini utekelezaji wake ni hafifu kiasi flani. Ni kweli kwamba kuna tatizo la rasilimali Pesa katika nchi yetu maskini yenye rasilimali kibao, lakini kama kweli tunaimba huu wimbo wa kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa ni lazima tuhakikishe kwamba pesa inayohitajika kwenye kilimo itoke katika pesa ya ndani, na syo kutoka kwa wahisani ambao wanatoa masharti ya jinsi ya kuzitumia kwa matakwa yao na ya nchi zao. Katika hili lazima wenye mamlaka wajue kwamba Tusikubali watu wetu washibishwe na Wazungu. Hebu sasa tujiulize kama watanzania, tuko wapi katika kilimo na tunataka kufika wapi? 
  Suluhisho la jambo hili ni kuhakikisha kwamba mkulima analima kwa tija na anapata soko la uhakika kwa kuwekewa mazingira shirikishi katika kilimo chake. Hayo ni maoni yangu, toa maoni yako ukimlenga mkulima na kilimo chake ukilinganisha na wimbo huu  "kilimo ndio uti wa mgongo wa taifa" Tuma maoni kwenye email  mmisungwi@gmail.com

SEKTA YA MIFUGO TANZANIA: SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU

SEKTA YA MIFUGO TANZANIA: SHUBIRI MWITU (ALOE) TIBA YA MAGONJWA YA KUKU: Shubiri mwitu (Aloe) ni mmea ambao umekuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mbalimbali ya binadamu na mifugo. Mmea huu unatumika sasa kutengen...

SEKTA YA MIFUGO TANZANIA: KILIMO KWANZA: KILIMO CHA KUTUMIA JEMBE LA KUKOKOT...

SEKTA YA MIFUGO TANZANIA: KILIMO KWANZA: KILIMO CHA KUTUMIA JEMBE LA KUKOKOT...: Ulimaji huu wa kutumia jembe linalokokotwa na ng'ombe ni kilimo cha tangu enzi za mababu, na kiasi kikubwa ndicho kimekuwa kikitumiwa...

MITIKI -KILIMO KWANZA: NG'OMBE - KWA TAARIFA YAKO

MITIKI -KILIMO KWANZA: NG'OMBE - KWA TAARIFA YAKO:  Ng'ombe mwenye afya kwa kawaida pua yake huwa na unyevu unyevu au kama vile inatoa jasho jembamba sana.Ukiona ng'ombe wako ana p...

Tuesday, November 5, 2013

MITIKI -KILIMO KWANZA: KILIMO BORA CHA MIHOGO

MITIKI -KILIMO KWANZA: KILIMO BORA CHA MIHOGO: Zao la muhogo ni  muhimu sana kwa Tanzania zaidi kwa wakulima wadogo wenye kipato cha chini. Wakulima wengi huchanganya zao la muhogo na...

Sunday, November 3, 2013

WAJANJA WA TOWN: KAMA ULIKUWA HUJAONA BASI ANGALIA HAPA MATOKEO YA ...

WAJANJA WA TOWN: KAMA ULIKUWA HUJAONA BASI ANGALIA HAPA MATOKEO YA ...: EXCLUSIVE: Matokeo Darasa la SABA 2013 haya hapa! Standard 7 2013 Exams Results Here... Kuangalia matokeo haya bofya   HAPA   kisha fuat...